DHANA YA UVAMIZI WA KIKOLONI
Uvamizi wa kikoloni
ni kitendo cha nchi moja kuingia katika nchi nyingine kwa lengo la kuanzisha
utawala wake kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Ø Mara
nyingi uvamizi huu hutekelezwa kwa kutumia nguvu za kijeshi.
Ø Uvamizi
wa kikoloni nchini Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) ulipingwa vikali kwa
sababu jamii za kitanzania zilifahamu kwamba kuruhusu wakoloni kuvamia
kungesababisha kupoteza uhuru wao.
Ø Kwa
sababu hiyo, viongozi wa jamii za kitanzania waliongoza mapambano dhidi ya
uvamizi huo tangu miaka ya 1880 na mapambano hayo yaliendelea hata baada ya
ukoloni kuanzishwa nchini Tanganyika.
Ø Mapambano
ya awali dhidi ya wakoloni yalihusisha jamii moja moja, yaani hayakuhusisha nguvu
za pamoja za jamii mbalimbali za kitanzania kama taifa moja la Tanzania.
Ø Mapambano
hayo yalilenga kuzuia kuingizwa kwa maadili ya kikoloni katika jamii za
kitanzania.
Ø Wakoloni
walileta maadili ya kibepari ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa rangi, uporaji,
ukatili, unyonyaji, unyanyasaji, matabaka, na ubinafsi.
Ø Pia
walileta maadili ya dini za kigeni (Ukiristo na Uislamu) ambayo mara nyingi
yalipingana na maadili ya dini za jadi
SABABU ZA KUPINGA UVAMIZI WA KIKOLONI NA
MAADILI YAKE
a)
Kupotea
kwa uhuru, kudunishwa na kuharibiwa kwa maadili ya jamii.
Ø Mila
na desturi ambazo zilikuwa msingi wa maadili ya kiafrika zilidhihakiwa na
wakoloni, hali hii ilichochea waafrika kuupinga uvamizi wa wakoloni ili kulinda
uhuru, utamaduni na maadili yao.
b)
Unyonyaji
na ukandamizaji wa kikoloni dhidi ya wananchi.
Ø Wananchi
walinyonywa kwa kulazimishwa kufanya kazi za vibarua na kulipwa ujira mdogo
katika mashamba ya mkonge, pamba, chai, tumbaku na pareto.
Ø Wakulima
hao walidhalilishwa kwa kuchapwa viboko wakiwa mashambani.
c)
Kuanzishwa
kwa mifumo mipya ya kodi kandamizi.
Ø Wakoloni
walianzisha mfumo wa ulipaji kodi kwa lazima, ikiwemo kodi ya kichwa, na
nyinginezo kwa pesa taslimu.
Ø Hivyo
wananchi iliwalazimu kuuza mifugo pamoja na kufanya vibarua katika mashamba yao
ili wapate pesa kwa ajili ya kulipa kodi hizo.
d)
Kuwepo
kwa adhabu za kikatili dhidi ya wananchi.
Ø Wakoloni
walianzisha adhabu za kikatili kama vile kuwanyonga viongozi wa jamii za
kitanzania waliopinga utawala na maadili yao.
Ø Wananchi
pia waliteswa na kudharirishwa hadharani waliposhindwa kulipa kodi au
walipotenda makosa mengine.
Ø Hali
hii ilishusha heshima na utu wao, jambo lililochochea harakati za kupinga
uvamizi wa kikoloni.
e)
Kuporwa
kwa ardhi yenye rutuba.
Ardhi ya wananchi iliporwa kwa ajili ya kulima mazao
ya biashara ya wakoloni, hali iliyofanya wananchi washindwe kukidhi mahitaji
yao ya chakula kutokana na kuwa na mashamba madogo yasiyo na rutuba ya kutosha.
f)
Kulazimishwa
kulima mazao ya biashara kwa faida ya wakoloni.
Pia wananchi walilazimishwa kulima mazao ya biashara
kama pamba, kahawa na chai kwa faida ya wakoloni na mabepari wa ulayamagharibi,
ambapo mazao hayo yaliuzwa kwa bei ndogo.
UPINZANI DHIDI YA UVAMIZI WA KIKOLONI KATIKA JAMII ZA KITANZANIA
Karibu
jamii zote za kitanzania ziliupinga uvamizi wa kikoloni kwa sababu hakuna jamii
iliyopenda kupoteza uhuru na utamaduni wake kwa wageni.
Uvamizi
huo ulipigwa kwa njia ya vita, zingine kwa kujisalimisha na nyingine kwa
kuungana na wavamizi
1.
NJIA YA KUPAMBANA KWA VITA
Ø Njia
ya vita ilikuwa maarufu zaidi kati ya jamii za kitanzania, kwani jamii nyingi
hazikuwa tayari kupoteza uhuru wao na hivyo ziliupinga waziwazi uvamizi huo kwa
kutumia vita.
Ø Mapambano
dhidi ya uvamizi wa kikoloni na maadili yake yalihusisha jamii moja moja au
jamii nyingi kwa pamoja.
(a)
Mapambano ya wanyamwezi
Ø Harakati
za kupinga uvamizi wa wajerumani magharibi mwa afrika mashariki ziliongozwa na
mtemi wa Wanyamwezi aliyejulikana kama Isike au Mwana Kiyungi kuanzia mwaka
1886 hadi 1891.
Ø Mtemi
Isike alipinga vikali uvamizi wa wajerumani katika himaya yake baada ya maeneo
yake ya kiutawala kuporwa. Pia alitetea masilahi ya kibiashara miongoni mwa
jamii ya kinyamwezi huko Tabora.
Ø Mtemi
Isike aliwaongoza kwa ushupavu askari wake kupambana na wajerumani wenye
wanajeshi zaidi ya 1000.
Ø Hata
hivyo ngome ya Isike ilivunjwa na wanajeshi wa kijerumani, na mtemi huyo
alipoona ameelemewa aliona ajiue kuliko kukamatwa na wajerumani, hivyo
alijilipua na baruti pamoja na familia yake mnamo mwaka 1893.
(b)
Mapambano ya jamii za watu wa Pwani
Ø Katika
ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki mapambano ya awali dhidi ya uvamizi wa
kijerumani yaliongozwa na wafanyabiashara mashuhuri ambao ni:-
i.
Abushiri bin Salim al-Harthi wa Pangani
ii. Bwana
Heri bin Juma wa Uzigua.
Ø Viongozi
hawa waliongoza mapambano dhidi ya sera za unyonyaji za kijerumani.
Ø Mwaka 1889, Abushiri bin Salim
aliwaongoza wananchi wa pwani katika maeneo ya pangani kupigana na wajerumani
na kufanikiwa kuwaondoa katika baadhi ya maeneo ya pwani.
Ø Wajerumani
hao waliomba msaada kwa majeshi ya uingereza, hali iliyosababisha Abushiri
kukimbia kwa sababu za kiusalama.
Ø Wajerumani
walifanikiwa kumkamata Abushiri baada ya kusalitiwa na chifu Magaya wa Usagara.
Mwaka 1889, Abushiri aliuawa kikatili kwa kunyongwa hadharani na wajerumani
huko bagamoyo
Bwana Heri
aliwaongoza wazigua maeneo ya Saadani dhidi ya uvamizi wa wajerumani.
Ø Ingawa
baadae alishindwa, alionesha mapambano makali ambayo yalionesha jinsi wananchi
walivyokuwa hawako tayari kunyanyaswa na kunyonywa na wajerumani.
Ø Kilwa
Kivinje, mapambano dhidi ya wajerumani yaliongozwa na Hassan bin Omari Makunyanga mwaka 1894.
Ø Hata
hivyo makunyanga alikamatwa na kunyongwa na wajerumani huko kivinje kwenye
mwembe ambao mpaka sasa unajulikana kama ‘mwembe wa kunyonga’
(c) Mapambano ya wahehe
Ø Jamii
ya wahehe chini ya uongozi wa Mtwa Mkwawa ilipinga vikali uvamizi wa wajerumani
kati ya mwaka 1891 na 1898 kwa njia ya vita.
Ø Wahehe
walijiimarisha sana kwa kupanua maeneo yao na kutoza ushuru kwa wafanyabiashara
waliopita kwenye maeneo yao.
Ø Wajerumani
walikasirishwa na kitendo cha wahehe kuendelea kujiimarisha kwa kuongeza maeneo
kama usagara, mpwampwa na ugogo.
Ø Wahehe
walikuwa wanaendeleza nguvu zao kutoka Kalenga, ambayo ilikuwa ngome ya Mtwa
Mkwawa hadi maeneo mengine.
Ø Mapambano ya kwanza ya kijeshi
kati ya wahehe na wajerumani yalifanyika mwaka 1891 katika eneo la Lugalo.
Wanajeshi wa kijerumani chini ya kamanda Emil Von Zelewisky walitumwa
kuangamiza wahehe.
Ø Katika
mapigano hayo, wanajeshi wa kijerumani walishindwa, takribani askari 300 wa kijerumani pamoja na kiongozi wao waliuawa.
Ø Mwaka
1894, wajerumani chini ya kamanda Tom Prince walivamia ngome ya wahehe huko
Kalenga. Mkwawa alikimbilia mafichoni na kuendelea na vita vya msituni.
Ø Mwaka
1898, Mtwa Mkwawa aliamua kujiua kwani aliona ni fedheha kwa shujaa kukamatwa
na kunyongwa hadharani na wavamizi.
(d) Mapambano ya wayao
Ø Kwa
upande wa kabila la wayao mapambano yaliongozwa na kiongozi wao jasiri na
shupavu aliyeitwa Mwene Machemba.
Ø Kiongozi
huyu alishinda karibu mapambano yote aliyoyaongoza dhidi ya wajerumani.
Ø Mwene
machemba alikuwa kiongozi hodari, shupavu na mwenye kupenda kutetea maadili na
uhuru wa watu wake.
Ø Kwa
mfano katika barua aliyowaandikia wajerumani, Mwene
Machemba alisema ‘’nimesikiliza
maneno yenu, lakini sijaona sababu ya kuwatii. Niko tayari kufa…, sisemi mnitii
mimi kwa kuwa nyie ni watu huru kama mimi’’
Ø Hata
hivyo Machemba alikimbilia msumbiji baada ya kupambana vikali na majeshi ya
kijerumani, ambapo wayao walizidiwa nguvu na kushindwa vita.
(e) Mapambano ya wachaga
Ø Katika
jamii ya wachaga, mapambano dhidi ya uvamizi wa kikoloni yaliongozwa na:-
i.
Mangi
Sina wa Kibosho
ii.
Mangi
meli wa Moshi.
Ø Huko
kibosho walipinga kitendo cha wajerumani kuingilia mgogoro uliokuwepo miongoni
mwa watawala wa Kibosho, Moshi na Marangu.
Ø Kitendo
hicho kilimuudhi Mangi Sina na kuamua kuichana bendera ya Wajerumani jambo lililowakasirisha
wajerumani, ambao walitumia majeshi ya kukodi ya wanubi kutoka Sudani ili
kupambana naye.
Ø Hata
hivyo, baada ya kuzidiwa nguvu na wajerumani, Mangi Sina alilazimika kutoroka.
Ø Mangi
Meli aliongoza mapambano huko Moshi dhidi ya majeshi ya kijerumani.
Ø Katika
mapambano hayo, Kamanda wa jeshi la wajerumani, Von Bulow, aliuawa.
Ø Kwa
kulipiza kisasi, wajerumani walimshambulia Mangi Meli, wakamkamata na baadaye
wakamnyonga kwa ukatili kijijini kwake.
(f) Vita vya Liti Kidanka dhidi ya wajerumani (1908-1910)
Ø
Wajerumani
walifika singida mnamo mwaka 1901.
Ø Wajerumani
walikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa wanyanturu, walioongozwa na mwanamke shupavu, Liti Kidanka, kupinga
uvamizi huo.
Ø Liti
kidanka hakutaka wajerumani watawale eneo ambalo sasa ni mji wa singida.
Ø Hivyo
aliongoza mapambano makali dhidi ya askari wa kijermani walioongozwa na Kapteni
Eberhard von Sick
Ø Liti
na askari wake walipambana na wajerumani mara mbili na kufanikiwa kuwakimbiza
nje ya mji wa singida kwa kutumia mbinu ya kipekee ya silaha ya nyuki wakali.
Ø Nyuki
walifunguliwa kipindi cha mapigano na kuwashambulia askari wa kijerumani pekee.
Ø
Mapigano
hayo yalidumu kwa miaka mitatu, kuanzia mwaka 1908 hadi 1910
Ø Hata
hivyo, katika jaribio la tatu na la mwisho, Liti Kidanka hakufanikiwa
kuwashinda wajerumani kutokana na kusalitiwa na mmoja wa washirika wake. Hivyo
alikamatwa yeye na mume wake na kuuawa. Kichwa cha shujaa huyu kilikatwa na
kupelekwa ujerumani.
(g) Mapambano ya jamii za kusini mwa Afrika mashariki ya
kijerumani (Vita vya maji maji)
Ø Mapambano
ya jamii za kusini, yajulikanayo kama vita
vya maji maji yalianza mwaka 1905 na kumalizika mwaka 1907.
Ø Kiongozi
wao alikuwa ni Kinjekitile Ngwale wa
kabila la wamatumbi, ambaye aliwaongoza wamatumbi kupinga ukatili, unyonyaji na
ukandamizaji wa wajerumani.
Ø Kinjekitile
alidai kuwa ameoteshwa dawa ambayo ingewaepusha na risasi za wajerumani.
Ø Dawa
hiyo ilikuwa ni mchanganyiko wa maji na mtama, yaliyodaiwa kuwa na uwezo wa
kuzigeuza risasi kuwa maji.
Ø Wanajamii
waliamini ahadi zake na vita ilipoanza, wakoloni waliporusha risasi, wao
walitamka maji, hata hivyo, kadri walivyosema maji ndivyo walivyopoteza maisha.
Ø Vita
hivi vilienea katika maeneo ya kusini na mashariki mwa afrika kama vile Rufiji,
Mohoro, Somanga, Kibata, Nandete, Mikindani, Liwale, Lindi, Songea, Njombe, na
Mahenge.
Ø Kinjengitile
alitumia mbinu hii kuwaunganisha na kujenga mshikamano miongoni mwa wananchi
ili wapambane na mkoloni bila hofu.
2.
KWA NJIA YA KUUNGANA
Ø Kuna
jamii za kitanzania zilijua nguvu ya kijeshi ya wajerumani na hawakuwa tayari
kupambana na kuupinga uvamizi wao moja kwa moja. Lakini waliungana ili kuweza
kuwashinda maadui wao.
Sababu za kuungana na Wakoloni.
i.
Imani
kwamba, baada ya kuwashinda maadui wao wa muda mrefu wangebaki kuwa na nguvu
zaidi na kujiimarisha.
ii.
Kupata
misaada ya silaha na vifaa vingine kutoka kwa wajerumani.
iii.
Nguvu
ndogo ya kijeshi kwa jamii za Kitanzania
Ø
Mfano
wa jamii hizi za kitanzania ni kama vile wachaga ambao walikuwa chini ya Mangi
Mandara waliungana ili kumshinda Mangi Sina, Wasangu na wabena waliungana na
wajerumani kupambana na Mtwa Mkwawa wa wahehe
Ø Ukweli
ni kwamba jamii hizi zote zilishindwa kupata walichokitarajia na mwisho
kutawaliwa kirahisi na wajerumani.
Ø Hivyo,
usaliti wao dhidi ya watawala wa jamii za kitanzania kwa kuungana na wajerumani
ulikuwa ni fedheha kwao kwani hakukuwa na manufaa yoyote.
3.
KWA NJIA YA KUSALIMU AMRI
Ø Kuna
baadhi ya jamii za kitanzania ambazo hazikupenda kutawaliwa na wakoloni lakini
zilijiona hazina uwezo wa kupambana nao kivita.
Sababu za kusalimu amri mbele ya Wakoloni.
i.
Atahari
zilizotokana na baa a njaa au magonjwa
ii. Ukosefu
wa dola zenye nguvu
iii.
Mazingira
magumu ya kivita n.k
Ø
Mfano
jamii za kimasai hapa nchini ilisalimu amri kwa wajerumani kufuatiwa kupatwa na
majanga ya magonjwa ya wanyama miaka ya 1870s na 1880s na mazingira yake
kutokuwa mazuri kwa vita
CHANGAMOTO
ZILIZOKABILI MAPAMBANO DHIDI YA UVAMIZI WA KIKOLONI
Ø Wananchi
walijaribu kupambana na kupinga ukoloni, lakini wakoloni waliwazidi nguvu na
kuwashinda.
Zipo sababu nyingi zilizowafanya wananchi kushindwa katika
mapambano hayo, miongoni mwa sababu hizo ni kama zifuatazo;
a)
Ukosefu wa umoja miongoni mwa jamii za
kitanzania.
Katika kipindi cha ukoloni, jamii za kitanzania
zilishindwa kwa sababu zilikosa umoja na hazikushirikiana kupambana na
wakoloni.
Ø
Kwa
mfano katika vita vya maji maji, makabila hayakuungana yote kwa pamoja kila
kabila lilipigana kivyake katika eneo lake
b) Matumizi ya silaha duni dhidi ya silaha bora za wajerumani.
Silaha zilizotumiwa na jamii za kitanzania zilikuwa duni
sana. Wajerumani walitumia mizinga na bunduki, wakati wananchi walitumia pinde,
mishale, ngao, mawe, marungu na majambia
c)
Usaliti.
Baadhi
ya viongozi wa jadi waligeuka kuwa vibaraka wa serikali ya kikoloni.
Ø
Mfano wasangu na wabena waliungana na
wajerumani kutoa siri na kupigana na wahehe. Vivyo hivyo katika jamii za kichaga Mangi Mandara/ Rindi
waliungana na wajerumani kumshinda Mangi Sina
d)
Maandalizi duni;
Wananchi hawakuwa na maandalizi mazuri ya vita
ikilinganishwa na wajerumani.
Ø
Wavamizi
walikuwa na muda mzuri wa kujiandaa kwa vita, wakati jamii nyingi za Kitanzania
zilijikuta katika vita ghafla baada ya kuona wavamizi tayari wameshaingia.
Ø
Pia
jamii za Kitanzania zilikuwa hazijamjua vizuri adui yao jambo lililochangia
kushindwa kwao.
e)
Teknolojia duni ya mawasiliano;
Watanzania
walitumia njia za jadi katika mawasiliano na zilitumia muda mrefu kufikisha
taarifa kwa walengwa. Hii ilipelekea ugumu wa mawasiliano wakati wa vita.
Ø Wajerumani
walikuwa na teknolojia nzuri ya mawasiliano na usafiri, ambayo ilirahisisha
mawasiliano kati ya maeneo mbalimbali, mfano matumizi ya telegram kutuma
taarifa za vita kuhusu vifaa na wanajeshi kwa haraka. Pia wajerumani walitumia
magari huku watanzania wakitembea kwa miguu.
f)
Uchumi dhaifu;
Ø Jamii
nyingi za kitanzania zilikuwa na uchumi dhaifu ambao usingeweza kuhimili vita
kwa muda mrefu.
Ø Wakati
huohuo Wajerumani walikuwa na uchumi imara uliowawezesha kuhimili vita kwa muda
mrefu kwani nchi ya ujerumani ilikuwa na uwezo wa kuwasidia kifedha.
MATOKEO YA KUPINGA UVAMIZI WA KIKOLONI
Ø Ni
muhimu kukumbuka kuwa jamii za kitanzania zilipambana vikali kuupinga ukoloni.
Kutokana na matumizi ya silaha duni za jadi, wakoloni walifanikiwa kuzishinda
na kuzitawala. Katika kipindi chote cha vita, wananchi walijitoa kwa hali na
mali wakiongozwa na viongozi wao wa jadi waliotetea uhuru, haki, masilahi na
utu wao.
Matokeo ya mapambano hayo ni kama ifuatavyo
i.
Kusimama kwa shughuli za uzalishaji mali;
Kipindi
chote cha vita badala yz kuzalisha muda mwingi ulitumika kujipanga kivita na kupigana.
Ø Hali
hii ilisababisha upungufu wa chakula na kuleta njaa kubwa, njaa hii iliitwa ‘Fungafunga’ huko kusini kwenye vita vya
maji maji.
Ø Watu
wengi walikula wadudu, mizizi na matunda ya msituni ambayo baadhi yalikuwa na
sumu
ii.
Kutumikishwa kwa nguvu kazi ya vijana;
Wanaume
hasa vijana wenye nguvu walisafirishwa mbali na makazi yao na kutumikishwa
katika mashamba ya walowezi.
iii.
Watu kuyaacha au kuyakimbia makazi yao
Wakati wa vita, wapiganaji walitumia muda mwingi msituni.
Wanawake na watotot pia walikimbilia msituni na kwenye mapango ili kujificha.
Ø
Hali
hii ilipelekea wengine kujeruhiwa na wengine kuuawa na wanyama wakali wa
msituni
iv.
Hofu miongoni mwa watanzania;
Vita
vilisababisha kujengeka kwa hofu miongoni mwa watanzania. kutokana na kushindwa
kwa mapambano, watu wengi walipata hofu ya kupigana tena na wazungu jambo
ambalo lingepoteza uhai wao.
v.
Mateso na vifo vingi vya watu.
Vita vya kupinga uvamizi wa wakoloni vilisababisha maelfu
ya vifo vya watu katika mapambano, kukamatwa kwa mateka, kunyongwa nakadhalika.
Ø
Pia
baadhi ya vifo vilitokana na njaa wakati na baada ya vita.
vi. Mwamko mpya wa harakati za uhuru;
Baada
ya kushindwa kwenye vita hivo, jamii nyingi za kitanzania zilionesha ujasiri na
dhamira ya kweli ya kupinga ukandamizaji wa kigeni.
Ø Hali
hii ilichochea mwamko mpya wa wapigania uhuru wa baadae, ambao walijifunza
mengi kutoka kwa harakati hizo za kitaifa za kudai uhuru
vii.
Kumbukumbu muhimu katika historia ya Tanzania;
Vita
vya kupinga ukoloni ni kumbukumbu muhimu katika historia ya Tanzania
inayostahili kuheshimiwa na yeyote anayethamini utu, uhuru, haki, heshima na
usawa.
Ø Vita
hivyo ni kielelezo halisi cha Watanzania katika kukataa utawala wa kikoloni.
Ø Vita
hivyo vinatukumbusha kuwa tunapaswa kuwa na ushujaa na uzalendo kama ilivyokuwa
enzi za mababu na mabibi zetu.
ZOEZI
1)
Tofautisha
kati ya maadili ya kikoloni na maadili ya jamii za kitanzania
2)
Eleza
sababu tano (5) za kushindwa kwa mapambano ya awali ya jamii za kitanzania
dhidi ya uvamizi wa kikoloni
3)
Eleza jinsi
viongozi wa sasa wanapaswa kutetea masilahi ya wanachi kwa ujasiri na uzalendo
MADA YA KWANZA:UKOLONI KATIKA JAMII ZA KITANZANIA
MADA YA PILI:UKOLONI KATIKA JAMII ZA KITANZANIA
MADA YA TATU: MAPAMBANO YA AWALI DHIDI YA UVAMIZI WA KIKOLONI
MADA YA NNE: HARAKATI ZA KUDAI UHURU WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

No comments:
Post a Comment