DHANA YA MAADILI WAKATI WA UKOLONI
Ø
Dhana
ya maadili wakati wa ukoloni inahusisha mifumo ya kiutawala, kisiasa, kiuchumi
na kiutamaduni ambayo ililetwa na wakoloni pamoja na ile iliyokuwepo kabla ya
ujio wa wakoloni katika jamii za kitanzania
Ø Waafrika
waliendelea kuziishi mila na desturi zao, ingawa pia waliyapokea maadili mapya
kama vile imani za kiroho, mifumo ya kiutawala na tamaduni za kigeni.
Ø Ukoloni
ulipoingia na kujiimarisha, uliingiza mifumo mipya ya kimaadili na kijamii,
ambayo mara nyingi ilikinzana na mila za wenyeji.
Ø
Mifumo
hiyo ililenga kudhoofisha mila na imani za kiasili, zikiwemo dini za jadi na
mila na desturi zao
MAADILI YA JAMII ZA
KITANZANIA WAKATI UKOLONI UNAINGIA
Ø Katika
jamii za kitanzania, misingi ya maadili ilijengwa juu ya umoja, ushirikiano, na
mshikamano miongoni mwa wanajamii.
Ø Vilevile
utunzaji wa mazingira, heshima kwa wazee na viongozi vilikuwa ni sehemu muhimu
ya maadili hayo.
Ø Aidha
nidhamu, uaminifu na utii wa mila, miiko na desturi za jamii zilikuwa nguzo kuu
za maadili.
Ø Hata
wakati wa ukoloni, misingi hii iliendelea kudumishwa kwa kiasi kikubwa licha ya
changamoto zilizokuwepo
Ø Hali
ya maadili ya jamii za kitanzania wakati wa ukoloni unaingia imejipambanua
katika Nyanja mbalimbali ikijumuisha vipengele mbalimbali.
1)
Mila na desturi
Wakati
wa kuingia kwa ukoloni, jamii za kitanzania zilikuwa na mifumo thabiti ya
maadili iliyoongozwa na kanuni, miiko, mila na desturi zao.
Ø Maadili
kama vile uvumilivu, ukarimu, heshima kwa wazee na mamlaka, uadilifu,
kujitolea, usawa, na uwajibikaji yalikuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku
Ø Vilevile
jamii za kitanzania zilikuwa na utajiri mkuba wa mila, desturi, kanuni, miiko
na utaratibu uliorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Ø Mfano
wazee waliheshimiwa sana na walitumika katika ushauri, kufundisha ujuzi wa
kitamaduni na maamuzi ya mambo
mbalimbali katika jamii.
2)
Dini za jadi
Wakati
wa ukoloni ulipoingia, dini za jadi zilikuwa na nafasi muhimu katika kuunda
maadili ya jamii.
Ø
Watu
waliamini katika nguvu za asili, mizimu na miungu.
Ø
Maadili
ya dini za jadi yalisisitiza ushirikiano, upendo, heshima na umoja kwa
wanajamii.
Ø
Dini
za jadi zilitumika kusimamia maadili katika jamii, mfano waliokaidi maagizo
waliadhibiwa kwa njia mbalimbali kama vile mizimu.
Ø
Vilevile
matatizo mbalimbali katika jamii yalitatuliwa kwa njia za kiimani kupitia
matambiko na mbinu nyingine zilizohusiana na dini za jadi
3)
Utawala wa jadi
Wakati
ukoloni ulipoingia, jamii za kitanzania zilikuwa zikiongozwa na mifumo ya jadi
iliyotofautiana baina ya kabila moja na lingine.
Ø Majukumu
yote ya uongozi yalitekelezwa na machifu, wazee na mabaraza ya wazee.
Ø Uamuzi
wa viongozi hawa uliheshimiwa na watu wote katika jamii.
Ø Maamuzi
yalifanywa kwa faida ya jamii nzima na wala sio kwa masilahi ya wachache, dhana
ya utawala ilikuwa imefungamana kwa karibu na utamaduni na maadili ya jamii,
ikisisitiza uwajibikaji wa pamoja, heshima, na utii kwa mamlaka, uzalendo na
ustawi wa jamii nzima.
Ø Mifumo
ya kijadi ya utawala kama vile nyarubanja, ubugabire na umwinyi ilikuwa na
nguvu kubwa na ilijitokeza katika jamii kama wahaya, waha na jamii za pwani
mtawalia.
4)
Lugha na mawasiliano
Jamii
za kitanzania zilikuwa na aina nyingi za lugha za asili, ambazo kwa kiasi
kikubwa zilitokana na makabila ya jamii iliyohusika.
Ø Lugha
hizo zilikuwa ni utambulisho mkubwa wa jamii hizo na zilitumika kuwasilisha
maarifa, maadili na utamaduni kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Ø Mfano
methali, hadithi na nyimbo za jadi zilikuwa na jukumu kubwa katika kufundisha
maadili ya jamii na kurithisha maarifa na historia
Ø Lugha
ilitumika kama chombo cha kuhamasisha watu kushiriki katika shughuli mbalimbali
za uzalishaji mali.
Ø Kulikuwa
na aina mbalimbali za ngoma ambazo zilikuwa ni zao la lugha kulingana na jamii
husika, Mfano;- Wanyasa walikuwa na ngoma
ya Mganda,
Wamakonde walikuwa
na ngoma ya Sidimba
Wazaramo
na Waluguru wakiwa na ngoma ya Mdundiko
Ø Ngoma
hizi zilitumika kama ishara ya mawasiliano na zilichezwa katika matukio muhimu
ya kijamii kama vile harusi, msimu wa mavuno, au kuashiria kuanza kwa msimu wa
kilimo.
5)
Simulizi na hadithi
Simulizi
na hadithi zilikuwa nguzo muhimu za mawasiliano katika jamii za kitanzania.
Kila jamii ilikuwa na aina yake ya masimulizi yaliyoakisi utamaduni wao.
Ø Baadhi
yao ni kama vile hekaya, methali, vitendawili na hadithi, ambazo zilitumika
kufundisha, kuendeleza na kurithisha maadili ya kitamaduni kutoka kizazi kimoja
hadi kingine.
Ø Mfano;-
Wahehe walitumia ushairi kama njia ya kuwasilisha ujumbe, kuwaelimisha vijana
na kuwaburudisha.
6)
Mavazi
Wakati
wa kuingia kwa ukoloni, jamii za kitanzania zilikuwa na mavazi ya asili
yaliyotengenezwa kwa kutumia malighafi za kiasili kama vile ngozi za wanyama,
majani na magome ya miti.
Ø
Vile
vile walivaa mapambo kama vile hereni na bangili.
Ø
Mavazi
haya yalikuwa utambulisho kwao na yaliheshimu utamaduni wa kabila au jamii
husika.
Ø
Katika
jamii za kisukuma, mavazi yao yalitengenezwa kwa ngozi za wanyama na nyuzi za
mimea kabla ya kuanzishwa kwa nguo za kufuma, nguo hizo ziliakisi shughuli za
kilimo na ufugaji ya jamii ya wasukuma.
Ø
Watawala
walivaa nguo maalumu tofauti na watu wao
Ø Katika
matambiko, wazee pia walikuwa na aina ya nguo zenye rangi husika walizozitumia.
v
Mavazi
na mitindo ya kikoloni iliingia na kuenea katika jamii za kitanzania.
Wamisionari, maofisa wa kikoloni na wafanyabiashara walileta aina mpya ya nguo
kama vile suruali, mashati, magauni na suti.
v
Vile
vile maeneo ya pwani na vituo vya biashara kama ujiji na tabora, ambako
biashara zilifanyika kati ya jamii za kitanzania na waarabu, mavazi kama kanzu,
baibui, makubadhi na vikoi yalikuwa maarufu.
v
Hata
hivyo, mavazi ya kitamaduni yaliendelea kutumika, hasa maeneo ya vijijini na
miongoni mwa wale waliopinga ushawishi wa wakoloni na tamaduni za ulaya
magharibi.
ATHARI ZA MFUMO WA UKOLONI KATIKA MAADILI YA
KITANZANIA
Kuingia
kwa mfumo wa kikoloni katika jamii za kitanzania kuliathiri mifumo ya maadili
ya kijamii, kiutamaduni, kisiasa, na kiuchumi. Athari hizo ni kama zifuatazo
A.
Athari
za kijamii
Elimu:
i.
Kuanzishwa
kwa mfumo rasmi wa elimu ya kikoloni.
·
Mfymo
huu ulifuata mfumo wa elimu na maadili ya kimagharibi na ulaya.
·
Mfumo
huu uliathiri elimu za kijadi kama jando na unyago.
ii.
Elimu
ya wakoloni iliharibu utamaduni wa kitanzania.
·
Hii
ni kwasababu wanafunzi walilazimishwa kufuata desturi za ulaya ikiwemo
kuadhibiwa pindi wanapoongea lugha zao za asili
iii.
Watumishi
waliofanya kazi katika shule hizo waliamuliwa kuvaa mavazi yaliyoelekezwa na
serikali za kikoloni
iv. Kutokea
kwa matabaka
Matabaka yalikuwa kati ya wasomi walioelimika na wale
ambao hawakupata elimu ya kikoloni. Kuwagawa Watanzania ilikuwa moja ya malengo
makuu ya wakoloni katika sera ya “Wagawe ili watawaliwe”
Afya
Ø Kabla
ya ukoloni, waafrika walikuwa wanatibiwa kwa dawa asili kama mitishamba. Dawa
hizi zilipatikana kwa urahisi katika maeneo yao.
Ø Kulikuwa
na wataalamu waliobobea katika masuala ya afya kama vile waganga wa mitishamba,
wakunga na ngariba waliokuwa na jukumu la kutibu na kuzuia magojwa.
Ø Vilevile
huduma za afya za jadi zilihusishwa na imani za jadi, ambapo matambiko
yalifanyika kutibu baadhi ya magonjwa
Ujio wa wakoloni ulileta mifumo mipya ya afya
i.
Walianzisha
hospitali na vituo vya afya kwa kutumia mtindo na mfumo wa ulaya magharibi.
ii.
Walileta
pia dawa tofauti na zile zilizokuwa zinatumiwa na waafrika.
iii.
Wataalamu
wa tiba asili walizuiliwa kufanya tiba zao na mara nyingi kukamatwa.
iv.
Kubeza
na kudunisha mfumo wa tiba asili kwa njia mbalimbali Mfano kudai kuwa tiba
asilia hazina msaada wowote kwani ni uchawi na ushirikina.
B.
Athari
za kiutamaduni
(i)
Kuathiriwa kwa dini za jadi.
Imani za kiasili kama vile kuabudu miungu na mizimu
katika mapango, mito na mabwawa, milima na majabali ziliathiriwa sana baada ya
ujio wa wakoloni ambao walikuja na dini ya ukiristo kupitia wamisionari pamoja
na uislamu.
Ø
Dini
za jadi za Kitanzania zilidharauliwa na kupigwa vita na wakoloni.
(ii)
Kuathiriwa kwa lugha za asili kama vile kimasai,
kisukuma, kichaga n.k.
Lugha hizi hazikuwa tu njia za mawasiliano, bali zilibeba
utambulisho, utamaduni, mila na desturi, miiko na kumbukumbu katika jamii
husika.
Ø
Lugha
hizo ziliharibiwa baada ya wakoloni kuanzisha lugha zao kama kingereza
zilizotumika katika kufundishia mashuleni.
Ø
Ujio
wa lugha za kikoloni ulidhoofisha matumizi ya lugha za asili.
(iii)
Mavazi:
Baada
ya ujio wa ukoloni, kulianza kujitokeza mabadiliko ya taratibu katika mitindo
ya mavazi. Mavazi ya kimagharibi kama vile suti, tai, magauni n.k yalianza
kuingizwa na kukubalika. Hii ilisababisha kudunishwa kwa mavazi ya kijadi.
Ø Vilevile,
katika maeneo ya pwani, hasa miongoni mwa jamii za waswahili, mavazi
yaliathiria sana na utamaduni wa kiarabu kutokana na karne nyingi za biashara
na mwingiliano.
Ø Kwa
kawaida wanaume wa kiarabu huvaa kanzu huku wanawake wakivaa buibui
(iv)
Kuanzishwa
kwa mfumo wa utawala wa sharia za kikoloni:
Baada
ya ujio wa utawala wa kikoloni, mifumo ya jadi ilibadilishwa na kuwekwa chini
ya mamlaka ya kikoloni.
Ø Hivyo
basi kuanzishwa kwa mifumo ya kisheria ya kikoloni kulileta mabadiliko makubwa
ambayo mara nyingi yalikuwa magumu kutekelezwa na jamii.
Ø Hivyo
sharia za kimila na desturi za jamii za kitanzania ziliwekwa pembeni na hivyo
kuvuruga mfumo wa maadili ya jamii na kijadi kwa kuvunja mamlaka za viongozi wa
jadi kama machifu na wazee wa kimila.
(v)
Kuathiriwa
kwa Mifumo ya familia na jamii.
Miundo
ya kiutamaduni ya familia katika jamii za kitanzania ilijumuisha familia pana,
zenye uhusiano wa kindugu na majukumu yaliyo wazi kwa kila mwanafamilia.
Ø Kuja
kwa ukoloni kuliathiri kwa kiasi kikubwa maadili na miundo ya familia na jamii
hizo.
Ø Mfano.
Uchumi wa kikoloni ulianzisha miradi mbalimbali iliyohitaji wafanyakazi, hii
ilisababisha wanaume kwenda kufanya kazi maeneo ya mbali jambo lililosababisha
utengano wa familia.
Ø Pia
wakoloni walileta maadili mapya kuhusu familia, ndoa na uhusiano wa kijamii.
Kwa mfano, ndoa za kiislamu na kikristo zilichukua nafasi ya ndoa za jadi
c. Athari za kiuchumi
Kuja
kwa wakoloni kuliathiri taratibu mbalimbali za uzalishaji mali katika jamii.
Kabla ya ukoloni, shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, biashara, uvuvi na
ufugaji zilifanyika kwa mujibu wa mila na desturi za kitanzania na kulingana na
mahitaji ya jamii husika.
i.
Unyang’anyi
na unyonyaji wa mali za waafrika.
Ø Ujio
wa wakoloni ulibadilisha mfumo mzima wa uzalishaji na umiliki wa mali. Watu
walianza kunyang’anywa mali zao kama vile ardhi.
ii.
Uzalishaji
wa mazao ya biashara kama vile pamba na kahawa.
Ø Uchumi
wa kikoloni uliweka msistizo kwenye Uzalishaji wa mazao ya biashara kama vile
pamba, kahawa, chai na karafuu ili kuzalisha malighafi kwaajili ya viwanda huko
ulaya magharibi.
iii.
Kutoweka
kwa Umoja na mshikamano uliokuwepo kabla ya ukoloni.
Ø Hivyo
mfumo mpya ulioletwa na wakoloni ulijenga jamii tegemezi na yenye mashindano
badala ya umoja na ushirikiano kama ilivyokuwa hapo awali.
Ø Hii
ilitokana na kuanzishwa kwa mfumo wa umiliki binafsi wa mali
iv.
Kuanzishwa
kwa uchumi unaoendeshwa na fedha.
Ø
Wakoloni
pia walileta uchumi unaoendeshwa na fedha.
HITIMISHO
v Kwa
mantiki hii, jamii za kitanzania zilianza kutoka kwenye misingi yao ya maisha
na kuingia kwenye misingi mipya ambayo ilitingisha na kuathiri mifumo ya asili
ya maadili
MAADILI YA KITANZANIA YALIYODUMISHWA WAKATI WA UKOLONI
Ø Maadili
ya jamii za kitanzania yaliendelea kudumishwa hata wakati wa ukoloni. Baadhi ya
maadili hayo ni kama yalivyoelezwa hapa chini.
(a)
Umoja na ushirikiano.
Ø Dhana
ya maisha ya jumuiya na uwajibikaji wa pamoja ilikuwa tunu kuu katika jamii
nyingiza kitanzania.
Ø Mfano,
miongoni mwa wachaga, kilimo cha jumuiya na kazi za pamoja na zilikuwa na
umuhimu mkubwa. Vitendo hivyo vilichangia kudumisha umoja na mshikamano wa
kijamii.
(b) Heshima kwa wazee.
Ø Licha
ya kuwepo kwa utawala wa kikoloni, jamii za kitanzania ziliendelea kuzingatia
kanuni za kiutamaduni zilizosisitiza heshima kwa wazee, mfano jamii za kizaramo
ziliendeleza maadili haya.
Ø Wazee
waliyumika kutoa ushauri, kufanya maamuzi, kulinda maarifa na mapokeo ya
kijamii.
(c)
Mifumo ya haki ya jadi.
Ø Jamii
nyingi za kitanzania ziliendelea kutumia mifumo yao ya haki ya jadi katika
kutatua migogoro. Kwa mfano, miongoni mwa jamii za wasukuma katika kanda ya
ziwa, kulikuwa na mabaraza ya kimila yaliyowajibika kusuluhisha migogoro ndani
ya jamii.
Ø Mabaraza
hayayalishirikiana na mfumo wa kisheria wa kikoloni lakini yalisalia kuwa
chombo muhimu cha kudumisha sharia na maadili ya kitamaduni
(d) Ukarimu.
Ø Jamii
a kitanzania zilijulikana kwa ukarimu wao na thamani hii iliendelezwa hata
wakati wa ukoloni. Jamii hizi ziliamini katika umuhimu wa kuwatendea wageni kwa
heshima na ukarimu.
(e)
Utii kwa mamlaka.
Ø Wakati
wa utawala wa kikoloni, heshima kwa uongozi wa ndani na miundo ya kimila
iliendelea kudumishwa.
Ø Heshima
hii ilienea pia kwa watawala wa kikoloni, ingawa mara nyingi iliambatana na
upinzani.
Ø Kwa
mfano, chini ya utawala wa kikoloni, jamii nyingi za kitanzania ziliendelea
kuwaheshimu viongozi wao wa kimila kama machifu, wazee na wakuu wa koo.
Ø Wachaga waliendelea kuwaheshimu machifu wao
waliojulikana kama Mangi.
(f)
Utamaduni wa
masimulizi.
Ø Uwasilishaji
wa historia, utamaduni na maadili kupitia masimulizi, hadithi, mashairi,
methali, na nyimbo ulibaki kuwa njia muhimu ya kuhifadhi historian na
utambulisho wa makabila au jamii mbalimbali za kitanzania.
Ø Maadili
haya yalikuwa muhimu kwa mifumo ya jamii za kitanzania
Ø Vilevile
mapokeo ya simulizi yaliwezesha jamii kudumisha utambulisho wao kwa kurithisha
hadithi, methali, nyimbo na ngano ambazo zilikuwa na urithi wao wa kitamaduni.
(g)
Mavazi.
Ø Jamii
mbalimbali zilichukua juhudi za kipekee kuendeleza na kusambaza maarifa ya
mavazi ya jadi kwa vizazi vilivyofuata, zikitambua umuhimu wa kuheshimu na
kudumisha utamaduni wao wa kipekee licha ya shinikizo kubwa la kuvaa mavazi
tofauti yaliyoletwa na wageni.
Ø Mavazi
ya asili yalienziwa kupitia matamasha, mikusanyiko na sherehe mbalimbali za
kijadi kama vile sherehe za mavuno, jando na unyago, harusi na tohara.
Ø Mavazi
ya ulaya magharibi yalijenga taswira ya ubora wa utamaduni wao, imani mpya,
nguvu, ustaarabu na usomi.
ZOEZI
1.
Eleza dhana ya ‘’ maadili’’ katika utamaduni wa Mtanzani
2.
Jadili nafasi ya vijana katika kukuza maadili kwa jamii ya Kitanzania
3.
Eleza jinsi sera za kikoloni zilivyochangia katika mabadiliko ya maadili ya
jamii za kitanzania
4. Eleza athari za dini za kigeni katika mila na desturi
za jamii za kitanzania
5. Eleza athariza diniza kigeni katika mila na desturi za
jamii za kitanzania
6. Nini athari za mfumo wa elimu ya kikoloni katika
maadili ya kitanzania
7. Fafanua mbinu mbalimbali zilizotumiwa na jamii za
kitanzania kupinga mifumo iliyokuwa inaathiri maadili yao wakati wa ukoloni
MADA YA KWANZA:UKOLONI KATIKA JAMII ZA KITANZANIA
MADA YA PILI:UKOLONI KATIKA JAMII ZA KITANZANIA
MADA YA TATU: MAPAMBANO YA AWALI DHIDI YA UVAMIZI WA KIKOLONI
MADA YA NNE: HARAKATI ZA KUDAI UHURU WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
MADA YA TANO: UJENZI WA TAIFA BAADA YA UKOLONI
MADA YA SITA: MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR

No comments:
Post a Comment