DHANA YA MAPINDUZI:
Mapinduzi
katika mktadha huu yanarejerea harakati za kubadili utawala wa kisiasa, ndani
ya muda mfupi kwa kutumia nguvu za kijeshi au nguvu za umma.
Ø Mapinduzi yanahusisha kuiondoa serikali au mfumo wa utawala uliopo na kuweka mwingine.
AINA ZA MAPINDUZI
Kuna aina kuu mbili za mapinduzi ambazo ni kama ifuatavyo
i. Mapinduzi ya kisiasa
ii. Mapinduzi ya kijeshi
i.
Mapinduzi ya kisiasa
Ø Ni
mapinduzi yanayofanywa kupitia nguvu za umma.
Ø Katika
mapinduzi haya, wananchi walio wengi na wanyonge huwaondoa watawala wachache
kwa kuzitumia nguvu za umma, mara nyingi bila kumwaga damu kwa kiasi kikubwa.
Ø
Wananchi
wanaweza kutumia njia za maandamano n.k
ii.
Mapinduzi ya kijeshi
Ni
mapinduzi ambayo hufanywa na jeshi kwa lengo la kuondoa utawala uliopo
madarakani kwa kutumia mapigano au mbinu za kijeshi
Mfano
wa mapinduzi ya kijeshi ni kama ifuatavyo
·
Mapinduzi ya kijeshi Misri yakiongozwa na
Kanali Gamal Abdel Nasser dhidi ya Mfalme Farouk I mwaka 1952
·
Mapinduzi ya kijeshi Ethiopia yakiongozwa
na Mengistu Haile Mariam dhidi ya Haile Selassie mwaka 1974
·
Mapinduzi ya Jenerali Iddi Amin Dada wa
Uganda dhidi ya Rais Milton Obote mwaka 1971
CHIMBUKO LA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR
Ø
Zanzibar
ilikuwa chini ya utawala wa kisultani hadi mwaka 1890.
Ø
Sultan
Seyyid Saidi alikuwa sultani wa kwanza kuongoza dola mbili, yaani Omani na Zanzibar akiifanya Zanzibar kuwa makao makuu ya himaya hizo.
Ø
Sultani
huyo alihamia Zanzibar akitokea Muscat, Oman mnamo mwaka 1840.
Ø
Mnamo
mwaka 1890, Zanzibar iliwekwa chini ya watawala wa Waingereza na ikatambulika
kama mahamia ya Uingereza au ‘’British Protectorate’’.
Ø
Katika
hali hiyo, waingereza walitumia utawala wa sultani katika kuitawala Zanzibar.
Waingereza walitoa uhuru kwa Zanzibar tarehe 10 Desemmba 1963.
Uhuru huu ulikuwa wa serikali ya mseto wa vyama vya ZNP
na ZPPP. Uhuru huu haukuungwa mkono na waafrika wengi maana waliona kuwa uhuru
umetolewa kwa waarabu badala ya wananchi wote
Ø
Mapinduzi
matukufu ya Zanzibar yalikuwa ni kilele cha harakati za mapambano ya ukombozi
wa wazanzibar.
Ø
Mapambano
haya yalikuwa ni matokeo ya uchaguzi na uhuru uliotolewa tarehe 10 Desemba 1963
chini ya serikali ya waziri mkuu Mohammed Shamte na Sultan Jamshid bin Abdullah
Al Said, uhuru ambao ulijulikana kama ‘’uhuru wa wachache’’,
Ø
Hivyo,
kufikia tarehe 12 January 1964, yalifanyika mapinduzi rasmi Zanzibar chini ya
uongozi wa mwanamapinduzi Sheikh Abeid Amani Karume, ambaye aliongoza Zanzibar
kuanzia mwaka 1964 hadi alipouawa tarehe 7 April 1972.
SABABU ZA MAPINDUZI
MATUKUFU YA ZANZIBAR
Ø 12 Januari 1964, mapinduzi matukufu ya Zanzibar
yalifanyika. Sababu zilizosababisha mapinduzi Zanzibar ni kama ifuatavyo;
A: SABABU ZA KISIASA
i.
Kuondolewa
kwa utawala wa wenyeji
Kabla
ya utawala wa waarabu, wazanzibari walikuwa na viongozi wao kama vile mwinyi
mkuu kwa upande wa Unguja na Makamandume kwa upande wa Pemba.
Ø Baada
ya kuja kwa utawala wa wageni hasa kipindi cha usultani wa Waarabu watawala wa
kienyeji waliondolewa katika utawala.
Ø Kuanzia
wakati wa usultani wa Waarabu hadi ukoloni wa waingereza, masilahi ya wenyeji
hayakuzingatiwa wala hayakupewa kipaumbele.
Ø Mfano;
Wenyeji hawakushirikishwa kwenye vyombo vya kutoa maamuzi au kuwa viongozi
serikalini.
ii.
Ubaguzi katika Baraza la kutunga sharia.
Vilevile kwenye baraza la kutunga sharia, Waafrika
wachache walipata nafasi ukilinganisha na Waarabu na Wahindi.
Ø
Hivyo
wajumbe hawa wachache hawakuweza kutetea masilahi ya waafrika walio wengi
Zanzibar.
Ø
Kwaiyo
Wazanzibar hawakupata uhuru wa kujitawala na kufanya maamuzi yao wenyewe.
iii.
Udanganyifu na vurugu za uchaguzi.
Chaguzi zote tatu zilizofanyika Zanzibar zilitawaliwa na
mizengwe iliyosababisha kukataliwa kwa matokeo.
Ø Mfano, Uchaguzi wa Julai, 1963 ambao ulimfanya Mohamed
Shamte kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanzibar ulionekana ni upendeleo na
kuendeleza ubaguzi.
B: SABABU
ZA KIJAMII
i.
Mfumo
wa kibaguzi wa kikoloni katika masuala ya kijamii.
Huduma
za kijamii kama vile elimu, maji, umeme na afya zilitolewa kwa ubaguzi.
Ø Kwa
mfano, Mwaka 1955, asilimia 14 ya bajeti ya serikali katika elimu ilielekezwa
kwenye shule za Wahindi wakati kipindi hicho Wahindi walikuwa asilimia 6 tu ya
wakazi wa Zanzibar.
Ø Huduma
za maji safi na umeme ziliimarishwa katika maeneo ambako Waarabu, Wahindi na
Wazungu waliishi.
Ø Hivyo
ubaguzi katika Nyanja mbalimbali ulileta chuki na kusababisha kuzuka kwa
Mapinduzi ya Zanzibar mnamo January, 1964.
ii.
Kutozingatiwa
kwa maadili ya wenyeji.
Maadili ya kuheshimu watu wa rika na tabaka
zote hayakuzingatiwa.
Ø Watu
walianza kuheshimiwa kutokana na vyeo na asili yao (rangi)
C: SABABU ZA KIUCHUMI
i.
Unyang’anyi wa rasilimali za wenyeji kama vile ardhi.
Ø
Wazanzibar
wengi walinyang’anywa ardhi yao yenye rutuba na kubaki vibarua katika mashamba
ya wageni.
ii.
Kutawala kwa Wahindi katika biashara.
Ø
Wahindi
walitawala biashara zote za jumla na rejareja madukani wakiwa pamoja na
Waarabu.
iii.
Kuathirika kwa shughuli kama vile kilimo, uvuvi na
ufugaji.
Ø
Ujio
wa wakoloni uliathiri shughuli nyingi za uchumi za wazanzibar kama vile kilimo,
uvuvi, ufugaji n.k. wakoloni walichukua rasilimali kama ardhi zenye rutuba,
minazi na mikarafuu kwa manufaa yao binafsi na ya ukoloni
MCHANGO WA
MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR
Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 yalileta
mabadiliko makubwa katika historia ya Zanzibar na yalikuwa na athari kubwa
katika ukanda wa Afrika mashariki na maeneo mengine. Mapinduzi hayo
yalisababisha kuondolewa kwa utawala wa kisultani na kuanzishwa kwa serikali
iliyoongozwa na wazalendo wa chama cha Afro-Shirazi Party (ASP), Chama
kilichoongozwa kwa misingi ya utu, haki na ustawi wa watu wote bila kuzingatia
tofauti za asili, hadhi u kabila.
Michango ya mapinduzi ya Zanzibar ni kama ifuatavyo;
a) Kujenga umoja
Mapinduzi yalisaidia kuvunja migawanyiko na chuki
zilizojengwa kutokana na hali ya ubaguzi katika jamii wakati wa ukoloni.
Ø
Hii
ilidhihirishwa pale ambapo rais wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar alipotangaza
wajumbe 29 wa baraza la kwanza la mapinduzi Zanzibar.
Ø
Baraza
hili lilikuwa na jukumu la kuunda upya taifa lenye umoja, haki na kuondoa
ubaguzi uliokuwa umeota mizizi kwa miaka mingi visiwani Zanzibar.
Ø
Lakini
pia mapinduzi ya Zanzibar yalichochea muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika
na hatimaye kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964
b) Kujenga mshikamano
Mapinduzi ya Zanzibar yalichangia kwa kiasi kikubwa
kuleta mshikamano baina ya wananchi.
Ø
Hii
ni kwa sababu ya kuundwa kwa serikali inayowakilisha makundi yote ya kijamii
pamoja na kuondoa mgawanyiko wa kikabila na kidini
Ø
Aidha
serikali ya mapinduzi Zanzibar ilipitisha kanuni za ujamaa na udugu ambazo
zilisisitiza usawa, umiliki wa pamoja wa rasilimali na mshikamano.
Ø
Huduma
za jamii kama vile elimu, afya na makazi zilitolewa kwa usawa bila kujali
rangi, kabila au dini.
Ø
Vilevile
mapinduzi ya Zanzibar yalichochea hisia ya fahari ya kitaifa, uzalendo na
kujitolea kwa manufaa ya wote, ambayo yameendelea kujenga mfumo wa maadili wa
taifa hadi sasa
c) Ujenzi wa maadili
Mapinduzi ya Zanzibar yalileta ukomo wa matabaka yote
yaliyokuwepo kati ya waarabu, wahindi na waafrika.
Ø
Serikali
mpya ilisisitiza umuhimu wa demokrasia, haki za binadamu, utu, usawa na ustawi
wa watu.
Ø
Hii
ilichangia katika kuhifadhi maadili ya jamii kama vile ushirikiano, usawa,
kuheshimiana na kusaidiana ambayo ni sehemu muhimu ya utamaduni na utambulisho wa
Mzanzibari.
Ø
Sambamba
na hayo, mapinduzi pia yalisaidia kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili.
Kiswahili kilikuwa lugha rasmi ya serikali na wananchi wote wa Zanzibar.
ZOEZI
1.
Bainisha
jitihada zingine zilizochukuliwa na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika
kuujenga umoja, usawa na mshikamano kwa jamii za wazanzibari.
2.
Eleza ni
kwa namna gani lugha ya Kiswahili imefanikiwa kuwaunganisha wazanzibari baada
ya mapinduzi
3.
Fafanua
namna mapinduzi matukufu ya Zanzibar yanavyoenziwa katika jamii ya sasa ya
watanzania.
MADA YA KWANZA:UKOLONI KATIKA JAMII ZA KITANZANIA
MADA YA PILI:UKOLONI KATIKA JAMII ZA KITANZANIA
MADA YA TATU: MAPAMBANO YA AWALI DHIDI YA UVAMIZI WA KIKOLONI
MADA YA NNE: HARAKATI ZA KUDAI UHURU WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
MADA YA TANO: UJENZI WA TAIFA BAADA YA UKOLONI
MADA YA SITA: MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR

No comments:
Post a Comment