DHANA YA UJENZI WA TAIFA:
Ujenzi wa taifa
ni mchakato unaohusisha juhudi za pamoja za kuunda taifa jipya lenye
utambulisho wake kupitia mifumo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni,
unaozingatia haki, usawa na demokrasia.
Ø Katika
taifa la Tanzania, mfumo huu ulijengwa juu ya misingi ya kifkra, kiitikadi,
falsafa na maadili ya jamii za Kitanzania.
Ø Harakati
za ujenzi wa taifa zilikuwa muhimu kwa sababu ukoloni uliacha jamii
iliyogawanyika, yenye ukosefu wa miundombinu muhimu, rasilimali watu na pia
tofauti za kiuchumi na kijamii miongoni mwa wananchi.
MIFUMO ILIYIJENGWA KATI YA MWAKA 1961 HADI 1966
Ø Uhuru
wa Tanganyika wa desemba 9, 1961, pamoja na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya
januari 12, 1964, yaliashiria mwanzo wa ujenzi wa mifumo mipya ya kisiasa,
kijamii, kiutamaduni na kiuchumi kwa taifa huru la Tanzania.
Ø Mifumo
hiyo ilijengwa chini ya Mwl JK Nyerere wa TANU pamoja na Abeid Amani Karume wa
ASP.
Ø Aidha
, umoja ,uzalendo, kujitolea na kupenda kazi vilikuwa miongoni mwa maadili
yaliyojengwa, yakiongozwa na kauli mbiu iliyotangaza vitu dhidi ya maadui
watatu:
·
umaskini,
·
ujinga
·
maradhi.
Ø Mifumo
ya kisiasa, kiuchumi na kijamii iliyojengwa katika kipindi hiki imefafanuliwa
vema katika sehemu zinazofuata.
KISIASA
1.
Tanganyika kuwa Jamhuri
Ø Tanganyika
ilikuwa Jamhuri mwaka 1962.
Ø Jamhuri
ni serikali ya watu yenye mamlaka kamili, inayoongozwa na Rais.
Ø Kabla
ya Tanganyika kuwa jamhuri, serikali ilikuwa inaongozwa na Mwalimu JK Nyerere
kama waziri mkuu , aliyekuwa chini ya mamlaka ya malkia wa uingereza, huku Gavana
wa kikoloni akiendelea kuwa kiongozi mkuu wa nchi, akimwakilisha malkia
Elizaabeth II wa Uingereza.
SABABU ZA TANGANYIKA KUWA JAMHURI
i.
Hitaji la kuwa na uhuru kamili wa serikali,
Ø Hii
ni kwa sababu kabla ya Tanganyika kuwa jamhuri, nchi ilikuwa na uhuru wa
bendera chini ya uongozi wa malkia wa uingereza akiwakilishwa na Gavana.
Ø Gavana
huyo aliendelea kutekeleza baadhi ya majukumu ya kiserikali hivyo kumfanya
waziri mkuu kukosa mamlaka kamili
ii.
Tanganyika
ilitaka kutambulika katika jumuiya za kimataifa kama nchi yenye uhuru kamili.
Ø Hivyo
kuwa jamhuri ilikuwa njia ya kufanikisha hilo, kwani iliwapa fursa ya kushiriki
katika mikutano ya jumuiya hizo za kimataifa kama nchi kamili.
iii.
Kupata
uwezo wa kuingia mikataba ya kimataifa kama nchi huru yenye mamlaka yake
kamili.
Ø Wananchi
walitakaSerikali ya jamhuri ili kuwa na uwezo wa kuingia mikataba ya kimataifa
kama nchi huru yenye mamlaka yake kamili.
iv.
Kuwaondoa
Wazungu katika nafasi za uongozi wa juu.
Ø Lengo
lilikuwa ni kuruhusu Watanganyika kushika madaraka ya uongozi katika taifa lao.
Ø Kwani
kabla ya kuwa jamhuri, Waingereza walikuwa bado wameshikilia nafasi za uongozi
hali iliyowafanya Watanganyika wajihisi kuwa bado wapo chini ya utawala wa
kikoloni.
v.
Kuwapa
uhuru wananchi na viongozi kujitawala na kuharakisha maendeleo ya taifa.
Ø Wananchi
wa Tanganyika walitaka kufanya maamuzi bila kuingiliwa na wakoloni, kwani
viongozi wa serikali hawakuwa na uhuru wa kufanya maamuzi ya kiutawala kabla ya
jamhuri.
HIVYO;
v Baada ya Tanganyika kuwa Jamhuri
mwalimu Nyerere aliunda baraza la mawaziri.
2.
Kuanzishwa kwa sera ya Afrikanaizesheni
Ø Hii
ni sera iliyowapa madaraka watanganyika na wazanzibari wazawa.
Ø Sera
hii ililenga kutoa nafasi za uongozi na ajira kwa wazawa ambazo awali zilikuwa
zikishikiliwa na wazungu na waasia wakati wa utawala wa kikoloni.
Ø Watanganyika
na wazanzibari wenye ujuzi walihamasishwa kufanya kazi serikalini na katika
mashirika ya umma.
3.
Kuanzishwa kwa mifumo ya ulinzi na usalama
Ø
Ulinzi
na usalama wa nchi pia ulitiliwa mkazo na serikali katika kujenga taifa.
Ø
Mfumo
huu ulianzia ngazi ya chini kupitia mfumo wa ubalozi wa nyumba kumi.
Ø
Ili
kuimarisha ulinzi na usalama, Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) liliundwa
mwaka 1964.
Ø
Tanzania
ilirithi jeshi la kikoloni lililojulikana kama King’s African Rifles (KAR)
ambapo nafasi nyingi za juu zilikuwa zikishikiliwa na wazungu na Waasia. Baada
ya uhuru, jeshi hili lilibadilishwa jina na kuitwa Tanganyika Rifles (TR) Hadi
mwaka 1964 lilipoanzishwa JWTZ.
Ø
Baada
ya kuanzishwa kwa JWTZ, serikali ikawa makini kuteua na kuchagua watu waliounda
jeshi jipya.
Ø
Kwa
sehemu kubwa, jeshi hili liliundwa na vijana watiifu, waadilifu na wazalendo
kutoka chama cha TANU na ASP. Bregedia Mirisho
Sam Hagai Sarakikya aliteuliwa
kuwa mkuu wa majeshi.
4.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Ø
Tarehe
26 Aprili, 1964, ni tukio muhimu la kihistoria na kisiasa katika kipindi hcho.
Ø
Muungano
huu ulitokana na uhusiano wa kihistoria uliokuwepo kati ya jamii za Tanganyika
na Zanzibar, uhusiano uliotokana na kiasi kikubwa cha udugu, historia na
biashara uliojengwa karne nyingi kabla ya ukoloni.
Ø Aidha, muungano huu ulikuwa nguzo muhimu katika kulinda
uhuru na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Muungano huu uliunda
utaifa mpya wa Utanzania.
5.
Uanzishwaji wa mfumo wa chama kimoja cha kisiasa mwaka 1965
Ø Tanzania
iliamua kufuta mfumo wa vyama vingi na kuanzisha mfumo wa chama kimoja.
Ø Vyama
vilivyoruhusiwa kufanya siasa ni TANU kwa Tanganyika na ASP kwa Zanzibar.
Ø Sababu
ya kuanzishwa kwa mfumo wa chama kimoja ilikuwa ni kuleta maendeleo na
kudumisha umoja na mshikamano. Uanzishwaji wa mfumo huu ulienda sambamba na
uanzishwaji wa siasa ya ujamaa na kujitegemea mwaka 1967
UCHUMI NA
HUDUMA ZA JAMII
Ø Mara
baada ya uhuru, serikali iliweka mkazo katika kujenga mifumo imara ya uchumi na
huduma za jamii.
Ø Harakati
za kujenga mifumo hii ziliongozwa na nadharia ya kupambana na maadui watatu:
·
Ujinga,
·
Maradhi
·
Umasikini.
UCHUMI:
Ø Mara
baada ya uhuru, Tanganyika na Zanzibar zilirithi mfumo wa uchumi wa kikoloni
ambao ulinufaisha watu wachache, hasa wageni.
Ø Maendeleo
yalikuwa ni hafifu katika sekta za biashara na viwanda.
Ø Kulihitajika
kujenga mfumo mpya wa uchumi. Mifumo ya uchumi iliyobuniwa katika kipindi hiki
ililenga kujenga jamii ya watu wanaojitegemea.
i.
Mpango wa maendeleo wa miaka mitatu
uliotekelezwa kuanzia mwaka 1961 hadi 1964.
ii.
Mpango
wa kwanza wa maendeleo wa miaka mitano (1964-1969).
iii.
Kuanzia
mwaka 1963, sera ya maendeleo ya vijijini ilianzishwa.
Ø Sera
hii ililenga kuwaweka wananchi katika vijiji ili kuimarisha kilimo kwa kutumia
teknolojia ya kisasa.
Ø
Wananchi
walihimizwa kulima mazao ya chakula na biashara. Kupitia uhamasishaji huu,
walipatiwa pembejeo na kupewa uhakika wa masoko ya mazao yao kupitia vyama vya
ushirika
Ø
Vile
vile viwanda mbalimbali vilijenga Tanganyika, mfano kiwanda cha nguo cha
urafiki mwaka 1966
Ø Aidha,
serikali ilijikita katika kuhakikisha taasisi za fedha zinaendelezwa ili kuwa
mihimili muhimu katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa. Serikali
ilianzisha benki kuu ya Tanzania mwaka 1966 ili kusimamia masuala muhimu ya
kifedha nchini. Pia sekta nyingine,kama uvuvi, nishati na mdini zilipewa
kipaumbele.
HUDUMA ZA JAMII
Ø Mabadiliko
katika utoaji wa huduma za jamii yalilenga kubadilisha mfumo wa kikoloni na
kuunda mfumo unaokidhi mahitaji ya taifa huru.
Ø Mfumo
mpya wa utoaji huduma za jamii ulilenga kujenga jamii yenye ujuzi , maarifa na
afya katika ujenzi wa taifa huru.
a.
Elimu.
Ø Serikali
iliandaa wataalamu wengi zaidi baada ya wazungu kuondoka
Ø Shule
nyingi zilijengwa na kuongeza idadi ya wanafunzi.
Ø
Elimu
ilitolewa kwa watu wote bila kujali jinsia, dini au kabila.
Ø
Vyuo
vya ufundi vilianzishwa, mfano chuo cha ufundi Dar es Salaam, ambacho
kilipanuliwa mwaka 1962 na kuanza kutoa elimu ya ufundi mwaka 1964.
Ø
Vyuo
vya ualimu pia vilianzishwa, mfano chuo cha walimu Morogoro.
b.
Afya
Ø
Zahanati
na hospitali za umma vijijini na mijini vilijengwa. Mfano hospitali ya
muhimbili ilipanuliwa zaidi mwaka 1961 mara tu baada ya uhuru.
Ø
Kuanzishwa
kwa program za mafunzo ya wahudumu wa afya na madaktari
Ø Serikali
ilijitahidi kuleta vifaa tiba na dawa kutoka nje ya nchi ili kuongeza ubora wa
huduma zilizokuwa zinatolewa.
v Juhudi
zote hizi ziliwezesha kuboresha hali ya afya kwa ujumla na kuweka mfumo wa afya
wakushughulikia changamoto mbalimbali za kiafya.
UTAMADUNI NA MAADILI
Ø Utamaduni
ni mfumo wa maisha unaojengwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine
kupitia malezi, elimu na mawasiliano ndani ya jamii.
Ø
Utamaduni
hujumuisha imani, maadili, mila na desturi, lugha, sanaa, muziki, mavazi
chakula na tabia zinazoainisha kundi fulani.
Ø
Serikali
baada ya uhuru ilifanya mambo yafuatayo ili kuimarisha utamaduni na maadili
miongoni mwa Watanzania.
a)
Kuifanya
lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya taifa.
Kiswahili
kilitumika kama njia ya kuhifadhi na kueneza maarifa, maadili na historia ya
jamii
b) Kuanzishwa
kwa vyombo mbalimbali vya kusimamia sanaa na michezo ili kulinda na kukuza
utamaduni wetu.
Ø Mfano
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Baraza la Michezo Taifa (BMT), Baraza la
Kiswahili la Taifa (BAKITA), Bodi ya
Filamu Tanzania, Makumbusho ya taifa na vyama mbalimbali vya kusimamia michezo
kama mpira wa miguu, pete, kikapu, ndondi na riadha
c) Sanaa
mbalimbali zilipewa kipaumbele kama vile uchoraji, uchongaji, ngoma na nyimbo.
d) Miziki
pia ilianzishwa, ambayo ilikuwa na lengo la kuelezea maadili na mapambano
yaliyofanywa kulikomboa taifa
e) Wasanii
na waandishi wa vitabu walihimizwa kutumia kazi zao kuelimisha umma kuhusu
ujenzi wa taifa.
MIKAKATI YA UJENZI WA TAIFA
Ø Kati
ya mwaka 1961 hadi 1966, serikali ya Tanzania iliweka mikakati mbalimbali ya
kujenga taifa linalojitegemea. Mikakati hiyo ni kama ifuatayo:
i. Kuanzishwa
kwa mfumo wa chama kimoja cha siasa.
Chama
cha TANU pamoja na ASP cha zanzibar ndivyo vilivyoruhusiwa kufanya shughuli za
kisiasa. Lengo la kufanya hivyo ni kuleta umoja na mshikamano baina ya
wananchi, kuondoa siasa za kibaguzi na kupunguza migogoro ya kisiasa.
ii. Kuondolewa
kwa mifumo ya uchifu katika uongozi wa nchi.
Lengo
ilikuwa ni kulijenga taifa upya. Machifu walikuwa na nguvu kubwa katika jamii
zao na mara nyingi walitumiwa na wakoloni kama vibaraka wao
iii. Kuanzishwa
kwa jeshi la kujenga taifa (JKT) tarehe 10 julai 1963.
Lengo ilikuwa ni kukuza uzalendo, maadili na ujenzi wa
taifa. Jeshi hili lililenga kutoa mafunzo ya kijeshi pamoja na stadi za kazi
kwa vijana wa kitanzania.
Baada ya miaka mitano ya uhuru wa Tanganyika, yaani 1966,
vitendo vya rushwa vilionekana kuongezeka na baadhi ya viongozi wa umma
walianza kujisahau.
Baadhi ya mambo yaliyojitokeza baada ya uhuru ni kama
yafuatayo:
a) Kujengeka kwa matabaka ya kiuchumi, kisiasa na
kijamii, kinyume na mfumo wa kijamii uliokuwepo kabla yauhuru ambapo jamii
iliishi kwa umoja,udugu,upendo na kushirikiana
b) Baadhi ya viongozi na watumishi wa umma walianza
kukiuka maadili ya utumishi wa umma na kutumia nafasi walizopewa kama vitega
uchumi ili kujinufaisha wenyewe
Ø Baada ya hayo kuanza kuonekana, serikali chini ya Mwalimu
JK Nyerere iliunda tume ya Rais ya Kudumu ya Uchunguzi (The presidential
Permanent Commission of Enquiry) ili kuchunguza mwenendo wa viongozi na
watumishi wa umma waliokuwa wakikiuka maadili, kujilimbikizia mali na kutumia
madaraka vibaya kinyume na miiko ya chama cha TANU.
CHANGAMOTO ZA UJENZI WA TAIFA
Ø Kipindi
cha mwaka 1961 hadi 1966 Taifa lilipitia changamoto mbalimbali za kiuchumi,
kijamii na kisiasa. Mfano, matumizi ya zana duni na ukosefu wa wataalamu katika
sekta ya kilimo,
Baadhi ya
changamoto zilizoathiri ujenzi wa taifa mara baada ya uhuru ni kama ifuatavyo:
a)
Uasi wa jeshi mwaka
1964
Ø Uasi
wa januari 20-27, 1964 pale Lugalo, ambapo kikundi kidogo cha wanajeshi wa
Tanganyika Rifles (TR) kiliasi na kutaka kuipindua serikali.
Ø Jaribio
hilo lilizimwa na waliohusika walipewa adhabu kali, kama kufukuzwa jeshini,
kufungwa na kuwekwa kizuizini kwa muda mrefu.
Ø Uasi
huu ulisababisha kuundwa kwa jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
b) Kuibuka kwa tabaka la mapepari uchwara
Ø
Kama
ilivyokuwa katika nchi nyingine nyingi za Afrika, tabaka jipya la mabepari
uchwara waliokuwa wamechukua madaraka serikalini walianza kutumia nyadhifa zao
kujinufaisha.
Ø
Wananchi
walianza kushuhudia viongozi wakiishi maisha ya anasa huku raia wa kawaida
wakibaki masikini.
Ø
Hali
hii ilikuwa tishio kwa umoja, maadili, amani na mshikamano uliokuwa
unasisitizwa na kujengwa mara baada ya uhuru
c)
Hali mbaya ya uchumi
Ø Katika
kipindi hiki, hali mbaya ya uchumi ilitokea na kuathiri sana upatikanaji wa
huduma za kijamii kama elimu, afya na nyinginezo zilizotolewa na serikali.
Ø Tatizo
hili lilisababisha pia ukosefu wa wataalamu , teknolojia duni, kuongezeka kwa
maradhi, ujinga na umasikini, pamoja na kuwepo kwa miundombinu mibovu.
Ø Hata
hivyo serikali ilianza kuchukua hatua za mageuzi ili kurekebisha changamoto
hizo
d)
Ukabila na migawanyiko ya kijamii
Ø
Kulikuwepo
na makabila mengi yenye mila na desturi tofautitofauti. Hali hii ilileta
changamoto katika kujenga umoja wa kitaifa, kuzuia siasa za kikabila n.k
e)
Changamoto au upungufu wa fedha.
Ø
Serikali
mpya ilikuwa haina mapato ya kutosha hivyo kutegemea zaidi misaada ya nje. Hali
hii ilipunguza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
f)
Elimu duni na ujinga.
Ø Katika
kipindi hiki, kiwango cha elimu kilikuwa cha chini sana kwakuwa shule zilikuwa
chache na watu wengi hawakujua kusoma na kuandika. Hali hii iliathiri uelewa wa
wananchi kuhusu maendeleo na utaifa.
g)
Athari za ukoloni
ZOEZI
1. Eleza jinsi tabaka jipya la mabepari uchwara
lilivyoathiri umoja na maadili ya kitaifa baada ya uhuru
2. Fafanua mikakati iliyochukuliwa na serikali baada ya
uasi wa jeshi wa januari 1964 ili kuimarisha usalama wa taifa
3. Fafanua umuhimu wa sera na mifumo ya kisiasa
iliyoanzishwa mara baada ya uhuru katika maendeleo ya kiuchumi na kisiasa kwa
Tanzania ya sasa
4.
Eleza faida za Tanganyika kuwa jamhuri
5. Ni maadili gani yalijengwa na kukuzwa wakati wa
ujenzi wa taifa, 1961 hadi 1996?
6. Ni njia gani bora zinazoweza kutumika kujenga na
kuimarisha umoja wa kitaifa wakati wa sasa?
7.
Pendekeza mikakati ya kuendelea na ujenzi wa taifa
la Tanzania wakati wa sasa
8. Ni kwa jinsi gani ngoma na nyimbo za jadi zinaweza
kutumika katika kujenga maadili na umoja wa kitaifa wakati wa sasa?
MADA YA KWANZA:UKOLONI KATIKA JAMII ZA KITANZANIA
MADA YA PILI:UKOLONI KATIKA JAMII ZA KITANZANIA
MADA YA TATU: MAPAMBANO YA AWALI DHIDI YA UVAMIZI WA KIKOLONI
MADA YA NNE: HARAKATI ZA KUDAI UHURU WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

No comments:
Post a Comment