KIDATO CHA NNE KISWAHILI
MUDA: Saa 3:00 Aprili, 2024
MAELEKEZO
1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B, na maswali mawili (2) kutoka sehemu C na swali la tisa (9) ni la lazima.
3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B ina alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30).
4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
5. Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU |
||
NAMBA YA SWALI |
ALAMA |
SAINI YA MTAHINI |
1 |
|
|
2 |
|
|
3 |
|
|
4 |
|
|
5 |
|
|
6 |
|
|
7 |
|
|
8 |
|
|
9 |
|
|
10 |
|
|
11 |
|
|
JUMLA |
|
|
SEHEMU A: (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Katika kipengele (i) - (x), chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye karatasi yako ya kujibia.
(i) Ubainishaji wa maneno ya kuzua au yasiyo rasmi katika lugha huhusisha alama ipi ya uandishi kati ya hizi?
A. Mkato B. Nukta-pacha C. Nukta
D. Nukta-mkato E. Mtajo
(ii) "Kiangazi kiliunguza kikaunguza....... Hatimaye, mwaka elfu moja mia tisa hamsini na sita mvua zikaanza ijapokuwa kwa maringo."Kauli hii inawakilisha aina gani ya hadithi?
A. Visasili B. Ngano C. Tarihi D. Soga E. Vigano
(iii) Kati ya methali zifuatazo, ipi ina maana tofauti na zingine?
A. Ujanja mwingi mbele giza.
B. Akili nyingi huondoa maarifa.
C. Mdharau biu huibuka yeye.
D. Ukupigao ndio ukufunzao.
E. Mdharau mwiba mguu huota tende.
(iv) Mbinu ya kufupisha maneno katika ushairi ili kupata ulinganifu wa mizani huitwaje?
A. Inkisari B. Tasfida C. Inkishafi
D. Tathilitha E. Ufupisho
(v) Katika masimulizi ya hadithi, maana sahihi ya soga ni ipi?
A. Hadithi fupi zinazoelezea makosa au uovu.
B. Hadithi fupi za kuchekesha na kukejeli.
C. Hadithi ndefu za kubuni na zinazochekesha.
D. Hadithi ndefu zinazohusu binadamu.
E. Hadithi zinazohusu binadamu na wanyama.
(vi) Katika neno 'umempelekea' mofimu ipi inawakilisha kauli ya kutendea?
A me- B -a
C -e- D -pelek-
E -m-
(vii) Kati ya maneno yafuatayo, neno lipi haliundwi kwa mbinu ya mwambatano?
A Batamzinga B. Jotoridi C Kataupepo
D Barabara E Mwanaanga
(viii) "Papai limeiva nyumbani lakini mashindwa kulila." Kauli hii inawakilisha aina gani ya
semi?
A Methali B Nahau C Misemo
D Kitendawili E Mizungu
(ix) Kulingana na chimbuko la Kiswahili, lahaja ya Kijomvu ilizungumzwa maeneo gani?
A Kaskazini mwa Tanga B Kusini mwa Somalia C Kisiwa cha Mafia
D Kisiwa cha Pemba E Sehemu ya Malindi
(x) Akija shule atanikuta. Katika tungo hii mofimu ki inaonesha dhima gani?
A Ukanushi B Uyakinishi C Masharti
D Umoja E Nafsi
2. Oanisha asasi zilizopo katika Orodha A na miaka ya kuundwa kwa asasi hizo iliyopo katika Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.
Orodha A |
Orodha B |
(i) Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (ii) Baraza la Kiswahili Zanzibar (iii) Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni Zanzibar (iv) Baraza la Kiswahili la Taifa (v) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (vi) Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni |
A 1979 B 2009 C 1970 D 2003 E 2012 F 1967 G 1972 H 1978 |
SEHEMU B (Alama 54)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. (a) Andika sentensi zifuatazo katika hali timilifu.
(i) Mimi ninamshinda Asha kwa mbio.
(ii) Peter hatawatembelea rafiki zake rikizo hii.
(iii) Wewe ni abilia lakini lazima ulipe nauli.
(iv) Mchezaji anarusha mpira.
(v) Mwalimu anafundisha somo la Kiswahili.
(b) Bainisha njeo sahihi katika tungo zifuatazo:
(i) Asha anafagia jikoni.
(ii) Mwalimu akiwafundisha kuimba wimbo.
(iii) John alikuwa amefika stendi.
(iv) Watoto wake watamlilia sana.
(v) Hapo nitakuwa nimeondoka.
(vi) Timu yetu ilicheza vizuri sana.
(vii) Askari wanalinda raia.
(viii) Watoto walikuwa wamemfurahisha.
4. (a) Eleza dhima tano za uambishaji katika lugha ya Kiswahili.
(b) Bainisha mzizi katika maneno yafuatayo:
(i) Mwokozi
(ii) Matendo
(iii) Mlaji
(iv) Uonevu
5. (a) Andika visawe vya maneno yafuatayo kisha tunga sentensi moja kwa kila kisawe.
(i) Majaliwa
(ii) Sahihi
(iii) Sifuri
(iv) Chuchumaa
(v) Mawio
(b) Eleza maana ya msingi na ya ziada kwa maneno yafuatayo:
(i) Mchumi
(ii) Husudu
(iii) Kichaa
(iv) Mchafu
6. Kwa kutumia hoja tano, eleza mambo yaliyochangia kukua na kuenea kwa Kiswahili kabla ya uhuru.
7. Soma simu ifuatayo kwa makini, kisha jibu swali linalofuata.
MAZOEA NGENGEMKENI SLP 150 BWIGIRI NJOO HARAKA BABA
MAHUTUTI MAINDA
Kutokana na simu hiyo, jifanye unasoma Shule ya Sekondari Makalo SLP 13 Njombe,
andika barua kwa mkuu wa shule kupitia kwa mwalimu wako wa darasa kuomba ruhusa
ya siku (8).
8. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata.
Lugha kaumba Mwenyezi, kusema na wake waja,
Lugha hubeba mapenzi, kufanya watu wamoja,
Maulana humuenzi, kubariki wake waja,
Lugha hakuna kitanzi, wawili huwa mmoja.
Lugha zote ni kamili, ijapokuwa hupungukiwa,
Hakuna mtu kamili, sembuse Lugha kukiwa,
Lugha uhuru kamili, hukataa kutawaliwa,
Lugha hukata kitanzi, wawili huwa mmoja.
Lugha yazidi dhahabu, hubeba utamaduni,
Lugha huzidi na lulu, kukupeleka mbinguni,
Kila lugha ni thawabu, kuwatoa utumwani,
Lugha hukata kitanzi, wawili huwa mmoja.
Lugha ni miundo mbinu, husafirisha mahaba,
Hufuta kabila zenu, kustawisha mahaba,
Toa tofauti zenu, lugha moja kuikaba,
Lugha hukata kitanzi, wawili huwa mmoja.
Maswali;
(a) Pendekeza kichwa kifaacho kwa shairi hili.
(b) Fafanua wazo kuu lilillobebwa na shairi hili.
(c) Kulingana na shairi hilo, lugha ina dhima gani?
(d) Eleza maana ya "kukata kitanzi" kama ilivyotumika katika shairi hilo.
(e) Katika shairi hilo kituo ni kipi?
(f) Unda habari ya maneno 50 kama kifupisho cha shairi hilo hapo juu.
SEHEMU C (Alama 30)
Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii. Swali la tisa (9) ni la lazima.
ORODHA YA VITABU
USHAIRI
Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi(EP & D. LTD)
RIWAYA
Takadini - Ben J Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N'tilie - E. Mbogo(H.P)
Joka la Mdimu - A. J. Safari (H.P)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
9. "Msanii yeyote wa kazi ya fasihi anafananishwa na Mwamvuli kwa jamii yake, kwa kuwa anatumia macho yake kuona maovu yaliyopo katika jamii na hutumia kalamu yake kuishauri na kuikinga jamii yake isipatwe na mabaya." Thibitisha kauli hii kwa kudadavua maovu matatu yaliyoibuliwa na waandishi kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
10. Waandishi mbalimbali wamemfinyanga mwanamke kwa namna tofauti, kwa kutumia hoja tatu kutoka kila diwani jadili kauli hii kwa kutumia vitabu viwili vya ushairi.
11. Kutokukubaliana miongoni mwa wanajamii kimekuwa chanzo cha mivutano mbalimbali kati yao na kupelekea kukosekana kwa amani, utulivu na utengamano katika jamii. Onesha ukweli wa kauli hii kwa kufafanua mivutano mitatu iliyojitokeza kutoka kila kitabu kati ya Tamthiliya mbili ulizosoma.
No comments:
Post a Comment