- Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
- Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
- Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
- Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
- Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
- Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
- Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule;
- Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Baiolojia kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulka na Serikali.
No comments:
Post a Comment