🧠 Ulishawahi kujiuliza… Data zikifutwa huwa zinakwenda wapi?
Ulishawahi kuformat flash drive (pen drive) halafu ukagundua umekosea?
Au flash yako iliwahi kugoma kusoma data zilizoko ndani yake kwa sababu ya virus, system failure, au kwa namna yoyote ile ukapoteza data zako muhimu?
Je, umewahi kufuta picha kwa bahati mbaya kwenye simu, flash drive, au hata kwenye kompyuta halafu ukaanza kujiuliza:
“Hizi data huwa zinakwenda wapi?”
Usijali! Leo nitakufundisha kidogo kuhusu jinsi data zinavyofutwa na namna ya kuzirudisha (recover) kwa kutumia programu moja maarufu sana iitwayo Disk Drill.
🔍 Kwanza: Data zikifutwa huwa hazifutiki kabisa!
Unapofuta faili, mara nyingi huwa hazipotei kabisa — mfumo wa kompyuta (OS) huondoa tu “alama ya mahali” faili lilipo. Kwa hiyo mpaka pale sehemu hiyo itaandikwa tena na data mpya, bado kuna uwezekano mkubwa wa kurecover(kuzirudisha).
🛠️ Namna ya Kurudisha Data kwa Kutumia Disk Drill
1. Pakua na Install Disk Drill
Pakua toleo la Windows au Mac, kulingana na kompyuta yako
Install kama programu nyingine ya kawaida au
2. Fungua Disk Drill
Programu itakuomba ruhusa ya admin — kubali.
Ukishaifungua, itaonyesha list ya disks (pamoja na flash drive yako ukishaichomeka).
3. Chagua Flash Drive au Disk yenye data iliyofutwa
Bofya flash drive au disk unayotaka kurudisha data.
4. Scan kwa Kutafuta Data
Bofya “Search for lost data”
Subiri programu ichunguze (inaweza kuchukua dakika chache kutegemea ukubwa wa diski)
Baada ya muda utaona mafaili mbalimbali yaliyoonekana
5. Preview na Chagua Mafaili
Unaweza kuona picha, video au document kabla ya kuzirudisha
Chagua unachotaka kisha bofya “Recover”
6. Hifadhi Mafaili Ulioyarudisha
Hifadhi kwenye disk tofauti na ile uliyozipotezea ili kuepuka kuandika juu data nyingine (overwriting)
⚠️ Angalizo Muhimu
Usitume data mpya kwenye flash/diski yenye data ulizopoteza kabla ya kuzirecover.
Usihifadhi mafaili uliyorecover kwenye sehemu ile ile.
Tumia deep scan kama quick scan haionyeshi mafaili unayoyatafuta.
💰 Toleo la Bure na la Kulipia
Unaweza kurudisha hadi MB 500 bure (Windows version).
Kwa zaidi ya hapo, unaweza kununua toleo la Pro kwa mara moja.
📌 Hitimisho
Ukipoteza data, usiogope!
Zipo njia salama na rahisi za kuzirejesha — Disk Drill ni miongoni mwa suluhisho rahisi na lenye nguvu kwa wanaoanza hadi wataalamu.
Ikiwa utahitaji maelekzo yakitaalamu zaidi, tucheck whatsapp kwa link hapa chini, tutakusaidia!
GET MORE PAST PAPERS WITH MARKING SCHEMES HERE
Get hired here Vacancies
GET THE MARKING SCHEMES FROM THE GROUPS BELOW
No comments:
Post a Comment