[ANWANI YAKO]
[TAREHE]
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Ndugu,
Yah: OMBI LA KAZI YA UALIMU III C – KISWAHILI MKOA WA RUVUMA
Rejea kicwa cha barua hapo juu.
Mimi Joyce Banda (20) mkazi wa wilaya ya Mbinga - Mkoa wa Ruvuma natumia nafasi hii kutuma maombi yangu ya ualimu (Mwalimu III C) katika somo la Kiswahili. Mimi ni mhitimu wa shahada ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 2022.
Kwa kutumia ujuzi nilioupata katika masomo yangu naamini ufanisi wangu katika kufundisha somo la Kiswahili utakuwa ni mkubwa na katika maadili ya fani yangu naya jamii kwa ujumla.
Kwa muda wa mwaka mmoja na nusu sasa nimekuwa nikijitolea katika shule ya sekondari Kalembo Mkoani Ruvuma na nimekuwa mahiri na mzoefu katika kufundisha somo hili la Kiswahili. Pamoja na mambo mengine, ninao uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo yote yanayohusu elimu.
Ninatumaini yangu kuwa ombi langu litapokelewa na kufanyiwa kazi.
Wako mtiifu,
[weka sahihi hapa]
Joyce Banda
Simu: [weka namba ya simu inayopatikana]
NB
Sehemu Zenye rangi nyekundu zibadilishe kuendana na taarifa zako, sehemu za blue jaza kwa kuweka taarifa zilizoelekezwa. Na sehemu zingine zijazwe kulinga na taarifa za mwombaji.
Hakikisha unasoma barua na CV yako kwa utulivu hadi mwisho kabla hujaituma.
See All Related Jobs | Visit Our Partner Site
GET PAST PAPERS WITH MARKING SCHEMES HERE
Get hired here Vacancies
No comments:
Post a Comment