Breaking

TOPIC 2: CHIMBUKO LA JAMII ZA KITANZANIA NA MAADILI YAKE | NOTES

CHIMBUKO LA JAMII ZA KITANZANIA NA MAADILI YAKE.

a. DHANA YA JAMII.

Jamii:
Ni mkusanyiko wa watu kwa ujumla wake.
Au
Ni watu pamoja na wanaume, wanawake na familia zao.
Au
Ni mkusanyiko wa watu ulioletwa kihistoria kwa ajili ya kuendeleza maisha yao na uzalishaji.


Jamii hujipatia katika vijiji, miji, nchi na mataifa kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile:
a. Uwindaji
b. Kilimo
c. Uvuvi
d. Ufugaji na
e. Biashara


Jamii inaundwa na makundi mbalimbali. Kundi la kwanza, ni watu wenye uhusiano wa damu au ndoa ambalo huitwa familia.

Familia:
Ni kikundi kidogo cha watu wenye uhusiano wa damu au ndoa kinachoundwa na baba, mama, watoto na ndugu wengine wa baba na mama.

Familia kadhaa zenye uhusiano wa damu na asili moja husunda kundi linaloitwa ukoo.

Ukoo:
Ni mkusanyiko wa familia zaidi ya moja zenye uhusiano wa damu na asili moja.

Kila ukoo huwa na kiongozi wake. Koo kadhaa zenye uhusiano huunda kundi kubwa linaloitwa kabila.

Kabila:
Ni kundi la watu wanaozungumza lugha moja na wana mila na desturi za asili moja.
Mfano wa kabila nchini Tanzania ni kama Sukuma, Gogo, Haya, Nyamwezi, Chaga, n.k.

Jamii za Kitanzania zimeishi na kupitia hatua mbalimbali za maendeleo na kimataifa kutoka Ujamaa, Ukabila na Ukapitali na Ujamaa.


2.2 Asili ya JAMII ZA KITANZANIA:

Jamii za Kitanzania ni mchanganyiko wa makabila mbalimbali yenye tofauti za muonekano, asili ya maisha na shughuli za kijamii na kiuchumi.
Tanzania inaundwa na makabila zaidi ya 120 ambayo yamegawanyika katika makundi makuu manne.
Makundi hayo ni Wakantu, Wakushiti, Wakhemu na Wanilo.

1. WABANTU:

Hii ni kundi linalojumuisha jamii nyingi za Watanzania wa leo asilimia 75 ya Watanzania wote.
Chimbuko la Wabantu wa Tanzania ni Afrika Mashariki katika eneo lililoko kusini mwa nchi za Kameruni na Nigeria.
Mfano wa jamii za Wabantu nchini Tanzania ni Wachaga, Wagogo, Waha, Wahadimu, Wahehe, Wanyakyusa, Wanyamwezi, Wapogoro, Wasukuma, Wazigua, n.k.

2. WAKHEMU:

Hii ni kundi la jamii ya wawindaji. Jamii hii imekuwepo Tanzania kabla ya Wabantu, hivyo ni watu wa asili wa Tanzania.
Mfano wa jamii ni Wasandawe na Hadzabe, wanaopatikana katika Bonde la Ufa katikati ya Tanzania na kaskazini ya Ziwa Eyasi.

3. WAKUSHITI:

Wakushiti ni Waafroasiatiki waliotoka maeneo ya Pemba ya Afrika katika nchi za Ethiopia, Eritrea na Somalia.
Jamii hii inajumuisha makabila ya Waarusha, Wapokomo na Wataturu.

4. WANILO:

Hii ni jamii ya wafugaji walioingia Tanzania wakiti wa kusini mwa Sudan. Asili yao ni kutoka Bonde la Mto Nile ambao wanatumia lugha ya Kinilo.


2.3 MTAWANYIKO WA JAMII ZA TANZANIA KABLA YA UKOLONI.

WAKHEMU:

Jamii hii ndio wazawa halisi wa iliyokuwa Tanganyika. Wanatumia lugha ya Kikhemu ambayo ni ya kigongagota ulimi. 

Shughuli kuu za uzalishaji mali za Wakhemu ni uwindaji na kukusanya matunda porini.

Mfano wa jamii hizo ni Wahadzabe na Wasandawe.

WAKUSHITO:

Wakushito wa Tanzania ya leo ni sehemu ya Wakushito wa kusini mwa Jangwa la Sahara ambao wengi wao ni Waraki na Wagorowa. Jamii hizi ni sehemu ya kusini mchanganyiko wa Waafrika na Waasia. Hawa walifika Ethiopia na shughuli zao za kiuchumi ni kilimo na ufugaji.
Wakushito wanahamia kaskazini mwa Tanzania katika harakati za kufuta maeneo ya kilimo na ufugaji.

WANILO:

Wanilo wa Tanzania ya leo ni sehemu ya jamii ya Wanilo wa kusini ambao hupatikana Afrika Mashariki katika nchi ya Tanzania, Uganda na Kenya. Kwa ujumla hii ni jamii ya Wadatoga na Wamaasai. Jamii kubwa ya Wanilo wa Tanzania ya leo ni Wamaasai.
Shughuli za kiuchumi ni ufugaji na kilimo.

WABANTU:

Wabantu kwa asili ni jamii iliyohama kutoka eneo lililipo kati ya Kameruni na Nigeria na kusambaa kusini mwa mashariki mwa Afrika.
Wabantu walisambaa kwa kuhama na kuingia Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania.


SABABU ZA KUTAWANYIKA NA KUHAMA.

  1. Mipasuko katika koo zao:
    Mipasuko ilikuwa jambo la kawaida katika jamii nyingi za kale. Hii ilibainishwa na mahitaji ya maisha kama vile chakula na malazi.

  2. Mabadiliko ya hali ya hewa:
    Kama vile ukame ambao uliathiri shughuli za kilimo na ufugaji.

  3. Kutafuta ardhi yenye rutuba:
    Kwa ajili ya kilimo na malisho ya mifugo.

  • Kuhamia huko kulileta mchanganyiko wa jamii na maendeleo mbalimbali kama vile:
    i. Kilimo
    ii. Ufundi
    iii. Matumizi ya chuma na
    iv. Kubadilishana bidhaa.

  • Wabantu wa Pwani walidhuriwa na utamaduni wa wageni kama vile Waarabu baada ya Karne ya 7. Ujio wa Waarabu uliathiri mila, desturi na utamaduni wa Wabantu na kuwafanya Waswahili.


A. WAHADIMU:

Hii ni jamii ya Wabantu wanaopatikana katika eneo la kati na kusini mwa kisiwa cha Unguja. Hadimu ni neno la Kiarabu "hasima" lenye maana ya kutoa huduma.

No comments:

Post a Comment