Kama sehemu ya kuendelea kurahisishaji kazi mashuleni, JIHUDUMIESCHOOL tumekuletea MFUMO WA MATOKEO ambao utatolewa bure kabisa kwa kila mtu!
Hakuna gharama zilizojificha wala taarifa za wanafunzi kutunzwa popote mtandaoni. Taarifa zote zinahifadhiwa kwenye browser ya mtumiaji tu!
🔗 Pata Mfumo Hapa:
👉 PAKUA MFUMO WAKO HAPA
Kwanini Utumie mfumo huu?
1. 100% Bure (100% Free Always) Mfumo huu ni wa bure kabisa. Hakuna malipo ya mwezi wala ya mwaka. Shule yoyote inaweza kujisajili na kuanza kutumia mara moja bila kikomo.
2. Usalama wa Taarifa (Data Privacy - Local Storage) Mfumo huu umejengwa kwa teknolojia ya kisasa inayolinda faragha yako. Mfumo HAUTUNZI taarifa za wanafunzi wala maksi zao kwenye server za mtandaoni. Vitu pekee vinavyohifadhiwa mtandaoni ni Jina la Shule (Username) na Nenosiri (Password) kwa ajili ya ulinzi wa akaunti yako. Taarifa zote za wanafunzi zinabaki na kuhifadhiwa kwenye kompyuta yako tu (Local Browser Storage).
3. Inafuata Viwango vya NECTA (Tanzanian NECTA Compliant) Mfumo unapanga madaraja (Divisions I - IV, 0), Posi (Position), na Points kiotomatiki kwa kufuata viwango na kanuni za Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Pia unatambua wanafunzi wasiofanya mitihani (ABS) na wenye masomo pungufu (INC).
4. Uchambuzi wa Kina wa Matokeo (Advanced Performance Analysis) Mfumo una tab maalum ya uchambuzi inayokupa taswira halisi ya ufaulu wa shule kwa kutumia:
Chati (Pie Charts & Bar Charts): Kuonyesha asilimia na idadi ya wanafunzi kwa kila daraja.
Orodha ya 10 Bora: Wanafunzi 10 waliofanya vizuri zaidi.
Orodha ya 10 wa Mwisho: Wanafunzi 10 wa mwisho ili kurahisisha ufuatiliaji.
Mwanafunzi Bora kwa Kila Somo: Inachambua na kutoa jina la mwanafunzi aliyeongoza kwenye kila somo.
5. Kutengeneza Ripoti Papo Hapo (Instant PDF Report Cards) Kwa kubonyeza kitufe kimoja tu, mfumo unatengeneza ripoti za wanafunzi wote zikiwa zimepangiliwa vizuri tayari kwa ku-print (PDF). Ripoti zinajumuisha Nembo ya Shule (Logo), Alama za Majaribio (CA), Alama za Mtihani (EXAM), Wastani, Madaraja, Maoni, na Tarehe za kufunga/kufungua shule.
6. Matumizi ya Lugha Mbili (Bilingual: English & Kiswahili) Mtumiaji anaweza kubadilisha lugha ya mfumo mzima muda wowote kati ya Kiingereza na Kiswahili. Ukibadilisha lugha, hata Ripoti (Report Cards) zinazozalishwa zitabadilika lugha na kusomeka kwa lugha uliyochagua.
7. Urahisi wa Kuingiza Maksi (Offline Excel Integration) Hakuna haja ya kuingiza maksi moja moja mtandaoni. Mfumo unakupa fomu ya Excel (Template), wewe unaijaza ukiwa offline, kisha unaipakia (Upload) kwenye mfumo na matokeo yote yanapangiliwa ndani ya sekunde moja.
8. Nidhamu na Maoni ya Waalimu (Behavior & Remarks) Mfumo unatoa nafasi ya kuweka daraja la nidhamu kwa kila mwanafunzi na kuchagua maoni (Remarks) ya Mwalimu wa Darasa na Mkuu wa Shule kwa urahisi sana kupitia orodha (dropdown) iliyoandaliwa tayari au kuandika maoni yako mwenyewe.
9. Customization (Kujibadilishia Taarifa) Shule ina uwezo wa kujipangia majina ya masomo yale tu wanayofundisha, kubadilisha viwango vya ufaulu (Grading System) kama wana viwango vyao vya ndani, na kuweka taarifa zote za shule.
⚠️ ANGALIZO MUHIMU SANA KWA WATUMIAJI (WARNING) ⚠️
Kama ilivyoelezwa kwenye sifa namba 2, mfumo huu unahifadhi maksi na majina ya wanafunzi ndani ya kivinjari chako (Browser Local Storage) kwa usalama wako, na SIO kwenye server za mtandaoni.
Hivyo basi:
"LAZIMA uhakikishe umepakua (Download) na kutunza vizuri faili zako za Excel zenye maksi za wanafunzi kwenye kompyuta yako. UKIFUTA TAKATAKA ZA BROWSER (Clear Browser Cache / Clear Browsing Data), taarifa zote za wanafunzi zilizokuwa zinaonekana kwenye mfumo zitafutika. Ikitokea zimefutika, utatakiwa kupakia (Upload) tena yale mafile yako ya Excel ili ziweze kuonekana na kutengeneza ripoti upya."
(Pia mfumo huu umebuniwa maalum kutumika kwenye Kompyuta (Desktop/Laptop). Ukifungua kwa simu, utakuomba ubadilishe simu yako iwe kwenye mfumo wa 'Desktop Mode' ili uweze kufurahia uwezo wake wote bila muonekano kubana).
🔗 Pata Mfumo Hapa:
👉 PAKUA MFUMO WAKO HAPA
📢 Shiriki na Wengine
Kama wewe kazi yetu hii imekupendeza, tafadhali share taarifa hii ili shule nyingi zaidi zinufaike na mfumo huu bure.
JIHUDUMIESCHOOL: Teknolojia bora + Elimu Bora = Taifa Imara
Anza Leo! Sahau shida ya kupanga matokeo na kuripoti kwa mikono. Tembelea

No comments:
Post a Comment