Breaking

Monday, 12 October 2026

DOWNLOAD JHS O-LEVEL RESULTS MANAGEMENT SYSTEM v1.5 FOR WINDOWS – TANZANIA SECONDARY SCHOOLS

Mfumo wa Kisasa wa Kutengeneza Matokeo ya Wanafunzi, Madaraja, Nafasi, Uchambuzi wa Matokeo na Report Cards kwa Shule za Sekondari Tanzania.

JIHUDUMIESCHOOL inakuletea JHS O-LEVEL RESULTS MANAGEMENT SYSTEM v1.5, programu ya kisasa ya Windows iliyotengenezwa mahsusi kusaidia shule za sekondari kusimamia, kuchakata na kuchambua matokeo ya wanafunzi kwa urahisi, haraka na usahihi.

Mfumo huu umeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya shule za sekondari Tanzania zinazotumia mtaala mpya, kuanzia Kidato cha Kwanza (Form One) hadi Kidato cha Nne (Form Four).

Badala ya kutumia muda mwingi kuhesabu wastani, kupanga nafasi, kutafuta madaraja na kuandaa ripoti za wanafunzi kwa mikono, JHS O-LEVEL inakusaidia kufanya kazi hizo kiotomatiki.

Programu ina muonekano wa kisasa, inaunga mkono lugha za Kiswahili na Kiingereza, na inaweza kutumika katika computer za Windows.


1. FEATURES OF JHS O-LEVEL RESULTS MANAGEMENT SYSTEM

A. Student Results Management

Mfumo unamwezesha mtumiaji kuingiza, kurekebisha, kuhifadhi na kuchakata matokeo ya wanafunzi kwa kila darasa na somo.

  • Kuingiza majina ya wanafunzi na jinsia.

  • Kuingiza alama za masomo mbalimbali.

  • Kurekebisha taarifa na alama za mwanafunzi.

  • Kupanga matokeo kwa kila darasa.

  • Kusimamia masomo tofauti kwa kila darasa.

  • Kutumia Excel katika kuingiza na kusimamia taarifa za matokeo.

B. Automatic Grading and Ranking

Programu inachakata alama za wanafunzi na kutoa taarifa muhimu za kitaaluma.

Mfumo unasaidia:

  • Kukokotoa madaraja ya masomo kiotomatiki.

  • Kupanga wanafunzi kwa ufaulu.

  • Kukokotoa division na aggregate.

  • Kukokotoa GPA na wastani wa ufaulu.

  • Kuonyesha alama pamoja na grade, mfano 64 - C.

  • Kuandaa takwimu za ufaulu kwa darasa na shule.

C. Division Summary and Performance Analysis

JHS O-LEVEL inatoa jedwali la muhtasari wa ufaulu linaloonyesha idadi ya wanafunzi waliopata Division I, II, III, IV, Zero na makundi mengine yanayotumika katika uchambuzi wa matokeo.

Muhtasari unaweza kuonyesha takwimu za wavulana, wasichana na jumla ya wanafunzi.

Pia mfumo unaonyesha:

CLASS AVERAGE | CLASS GRADE | CLASS GPA

GPA inaweza kuonyeshwa hadi nafasi nne za desimali, mfano 1.5053.



D. Automatic Student Report Cards

Mfumo unaweza kuandaa ripoti za maendeleo ya kitaaluma za wanafunzi, zikiwemo taarifa za masomo, alama, madaraja na maoni ya walimu.

Report Cards zinaweza kuangaliwa, kuchapishwa na kuhifadhiwa katika PDF.



E. Professional Printing and PDF Export

JHS O-LEVEL v1.5 ina mfumo wa Print Preview unaomruhusu mtumiaji kuangalia kurasa kabla ya kuzichapisha.

Vipengele vyake ni pamoja na:

  • Portrait na Landscape printing.

  • PDF Preview kabla ya kuchapisha.

  • Save as PDF.

  • Kuchagua font type na font size.

  • Kutumia Times New Roman, Arial, Calibri, Verdana au Georgia.

  • Kurekebisha ukubwa wa maandishi ya majina, alama na headings.

  • Kuchapisha results tables na division summaries katika mpangilio unaosomeka.

F. English and Kiswahili Support

Mtumiaji anaweza kuchagua lugha ya Kiswahili au Kiingereza kwa sehemu zinazounga mkono mabadiliko ya lugha.

G. School Registration and Login

Kila shule inaweza kusajili akaunti na kuingia kwenye mfumo kwa kutumia taarifa zake.

Mfumo unatumia online authentication kwa usajili na uthibitishaji wa akaunti, huku taarifa za kazi za shule zikihifadhiwa kwenye computer inayotumika.


2. SYSTEM REQUIREMENTS

Ili kutumia JHS O-LEVEL Results Management System, tunapendekeza computer yenye uwezo ufuatao:

RequirementRecommended Specifications
Operating SystemWindows 10 au Windows 11
Architecture64-bit (32-bit installer pia inapatikana)
ProcessorIntel pentium au inayolingana nayo au zaidi
RAM2 GB au zaidi; 4 GB inapendekezwa
Free Disk SpaceAngalau 500 MB
Display Resolution1366 × 768 au zaidi
Internet ConnectionInahitajika kwa usajili na online login tu
PrinterHiari, kwa kuchapisha ripoti
PDF ReaderInapendekezwa kwa kufungua PDF (kama una edge inatosha)

3. DOWNLOAD JHS O-LEVEL RESULTS MANAGEMENT SYSTEM v1.5

Pakua toleo linaloendana na computer yako.

DOWNLOAD FOR WINDOWS 64-BIT

JHS O-LEVEL Results Management System v1.5 – Windows 64-bit

DOWNLOAD 64-BIT JHS-O-LEVEL HAPA

Inapendekezwa kwa computer nyingi zinazotumia Windows 10 na Windows 11.


DOWNLOAD FOR WINDOWS 32-BIT

JHS O-LEVEL Results Management System v1.5 – Windows 32-bit

DOWNLOAD 32-BIT JHS-O-LEVEL HAPA

Kwa computer zenye Windows 32-bit zinazotumia toleo hili.

PORTABLE VERSION

JHS O-LEVEL Portable Edition – Windows 64-bit

PORTABLE VERSION (AVAILABLE UPON REQUEST ONLY)

Toleo la portable linaweza kuendeshwa bila installation ya kawaida baada ya kutoa mafaili kwenye ZIP.


4. HOW TO INSTALL JHS O-LEVEL ON WINDOWS

Fuata hatua zifuatazo ili kusakinisha programu kwenye computer yako.

STEP 1: Download the Software

Pakua Windows installer inayolingana na computer yako kupitia link zilizopo hapo juu.

STEP 2: Open the Setup File

Baada ya download kukamilika, fungua faili la JHS-OLEVEL-Setup-x64.exe au JHS-OLEVEL-Setup-x86.exe.

STEP 3: User Control

Chagua folder la kusakinisha programu pamoja na mipangilio ya kutengeneza Desktop Shortcut.

STEP 4: Terms & Conditions

Soma masharti ya matumizi ya programu na ukubali ikiwa unaridhia ili kuendelea.

STEP 5: Data Privacy & Protection

Soma sera ya faragha na ulinzi wa taarifa, kisha ukubali ili kuendelea na installation.

STEP 6: Developer & Contacts

Angalia taarifa za developer, mawasiliano na huduma nyingine zinazotolewa.

STEP 7: Complete Installation

Malizia installation na ufungue JHS O-LEVEL kupitia Desktop Shortcut.

Download Full Screenshots here


5. HOW TO USE JHS O-LEVEL RESULTS MA
13. 

12. 

11. 

10. 

9. 

8. 

7. 

6. 

5. 

4. 

3. 

2. 

1. 
SUPPORT 100% ANYTIME, ANYWHERE

NAGEMENT SYSTEM

Baada ya kufungua mfumo kwa mara ya kwanza, fuata mwongozo huu.

Step 1 – Register Your School

Ikiwa shule yako haijawahi kusajiliwa, bonyeza Create an Account na ujaze taarifa zinazohitajika.

Step 2 – Login

Ingiza jina la shule na password iliyosajiliwa. Internet inahitajika kwa online authentication.

Step 3 – School Details

Jaza au hakiki taarifa za shule, zikiwemo jina la shule na taarifa nyingine zinazohitajika.

Step 4 – Manage Classes

Tengeneza au chagua madarasa yanayotumika shuleni, kuanzia Form One hadi Form Four.

Step 5 – Manage Subjects

Weka masomo yanayofundishwa, kisha chagua masomo yanayohusika kwa kila darasa.

Step 6 – Enter Students and Results

Ingiza taarifa za wanafunzi na alama zao kwa kila somo. Pale inapowezekana, tumia Excel kurahisisha kazi.

Step 7 – Generate Results

Fungua sehemu ya matokeo ili kuona grades, rankings, division summaries na takwimu za ufaulu.

Step 8 – Generate Report Cards

Tengeneza ripoti za wanafunzi kwa kutumia data zilizoingizwa.

Step 9 – Print or Save as PDF

Chagua Portrait au Landscape, rekebisha font sizes ikiwa inahitajika, kagua Print Preview na uchapishe au hifadhi PDF.

[WEKA SCREENSHOTS ZA MATUMIZI YA MFUMO HAPA]


6. FREE TRIAL AND SOFTWARE ACTIVATION

JIHUDUMIESCHOOL inatoa nafasi kwa shule kujaribu programu kabla ya kulipia.

Mtumiaji mpya anapewa Free Trial ya siku 7 kuanzia siku ya installation, yenye uwezo wa kutumia premium features za mfumo.

Baada ya muda wa majaribio kumalizika, mtumiaji atahitaji activation key ili kuendelea kutumia mfumo.

OUR AFFORDABLE ACTIVATION PLANS

PlanPriceValidity
Free TrialTSh 0Siku 7
Yearly LicenseTSh 10,000Mwaka mmoja
Lifetime LicenseTSh 25,000Bila kikomo cha muda

Yearly License: Lipia TSh 10,000 kwa shule moja kwa mwaka mmoja.

Lifetime License: Lipia TSh 25,000 kwa shule moja, bila malipo ya renewal ya kila mwaka kwa leseni hiyo.

HOW TO ACTIVATE YOUR SOFTWARE

  1. Chagua Yearly au Lifetime Plan.

  2. Wasiliana na developer kupata maelekezo rasmi ya malipo.

  3. Fanya malipo kupitia Airtel Money kwa namba rasmi utakayopewa.

  4. Tuma uthibitisho wa malipo pamoja na jina la shule yako.

  5. Baada ya malipo kuthibitishwa, utapewa Activation Key.

  6. Ingiza key hiyo kwenye sehemu ya activation ya programu.

TUNAPENDA KUTOA HUDUMA KWANZA, MALIPO BAADAYE!

Ndiyo maana tumekuwekea siku 7 za kujaribu mfumo kabla ya kufanya uamuzi wa kulipia.


7. IMPORTANT INFORMATION ABOUT SCHOOL DATA

Taarifa za matokeo ya wanafunzi ni muhimu na zinapaswa kulindwa.

Watumiaji wanashauriwa kuhifadhi nakala za data zao mara kwa mara, kutunza passwords kwa usalama na kuhakikisha computer zao zinalindwa dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa.

Kwa kuwa mfumo unahifadhi taarifa za kazi kwenye computer inayotumika, hakikisha umehifadhi backup kabla ya kufanya formatting ya Windows, kubadilisha computer au kufuta data za programu.

Usifute school data folder bila kuwa na nakala salama.


8. WHY CHOOSE JHS O-LEVEL RESULTS MANAGEMENT SYSTEM?

JHS O-LEVEL imeandaliwa kurahisisha kazi za walimu, wakuu wa shule na watendaji wanaohusika na matokeo ya wanafunzi.

Mfumo unasaidia kupunguza muda unaotumika kufanya hesabu za matokeo kwa mikono, kurahisisha uchambuzi wa ufaulu na kuandaa ripoti zinazosomeka vizuri.

Unapatikana kwa gharama nafuu na una muonekano uliolenga matumizi ya shule za Tanzania.


9. OTHER SERVICES OFFERED BY JIHUDUMIESCHOOL

Mbali na JHS O-LEVEL Results Management System, tunatoa huduma nyingine za kutengeneza mifumo ya elimu na taasisi.

Huduma zetu ni pamoja na:

  • Mifumo ya kuandaa na kusimamia mitihani.

  • Primary School Management Systems.

  • Advanced Level School Management Systems.

  • School Payment Management Systems kwa shule za msingi na sekondari.

  • Library Management Systems.

  • Mifumo ya kutengeneza ripoti na kuchakata taarifa.

  • Custom Software Development kulingana na mahitaji ya mteja.

Tunaweza pia kutengeneza mifumo maalumu kwa shule, taasisi na biashara kulingana na mahitaji yao.


10. DEVELOPER & TECHNICAL SUPPORT

Developed by: JIHUDUMIESCHOOL

Developer: Baraka Loibanguti Mollel

Phone: +255 684 368 709

Email: itugnabiol@gmail.com

Website: https://www.jihudumieschool.com

Kwa maelezo zaidi kuhusu programu, activation keys, msaada wa kiufundi au kuagiza mfumo maalumu, wasiliana nasi.


FINAL WORDS

JIHUDUMIESCHOOL – WHERE EDUCATION IS FREE FOR EVERYONE.

Tunaamini kwamba teknolojia bora inaweza kuboresha usimamizi wa elimu na kupunguza kazi zinazochukua muda mwingi katika shule zetu.

Karibu utumie JHS O-LEVEL RESULTS MANAGEMENT SYSTEM v1.5.1, mfumo wa kisasa wa matokeo uliotengenezwa kwa mahitaji ya shule za Tanzania.

DOWNLOAD • INSTALL • REGISTER • ENTER RESULTS • ANALYZE • PRINT

JIHUDUMIESCHOOL — HUDUMA KWANZA, MALIPO BAADAYE!


No comments:

Post a Comment