JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA Makao Makuu ya Jeshi, Sanduku la Posta 194, Dodoma, Tanzania. 14 Aprili, 2026
NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHI
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshi kwa Vijana wa Kitanzania kuanzia elimu ya Sekondari hadi elimu ya Juu.
Vijana watakaoandikishwa Jeshi watapatiwa mafunzo mbalimbali muhimu ya Kijeshi na mafunzo ya kuwaendeleza katika taaluma zao.
SIFA ZA MWOMBAJI
Vijana wa Kitanzania wenye nia ya kuandikishwa Jeshi wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
Uraia: Awe Raia wa Tanzania wa kuzaliwa.
Umri: * Usiozidi miaka 25 kwa elimu ya Kidato cha IV na Kidato cha VI.
Usiozidi miaka 28 kwa elimu ya Juu.
Afya: Awe na afya nzuri na akili timamu.
Nidhamu: Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani au kufungwa.
Vyeti: Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate) na vyeti vya shule (Academic/School Leaving Certificates).
Ajira Nyingine za Usalama: Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo, Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo au chombo kingine chochote cha Ulinzi na Usalama.
Mafunzo ya JKT: Awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mkataba wa kujitolea miaka miwili (2) au Mujibu wa Sheria na kutunukiwa cheti.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe yalipokuwa Makao Makuu ya Jeshi Msalato Dodoma kuanzia tarehe 15 Aprili, 2026 hadi tarehe 28 Aprili, 2026 yakiwa na viambatisho vifuatavyo:-
Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au nambari ya NIDA.
Nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya Shule na Chuo.
Nakala ya cheti cha JKT kwa waombaji waliomaliza mkataba. Aidha, Vijana waliopo kwenye Makambi ya JKT hawahusiki na tangazo hili.
Nambari ya simu ya mkononi ya mwombaji.
Mkuu wa Utumishi Jeshini,
Makao Makuu ya Jeshi,
Sanduku la Posta 194,
DODOMA,
Tanzania.
Imetolewa na: Luteni Kanali Kevin Baraka Byabato Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

No comments:
Post a Comment