Breaking

Thursday, 21 March 2024

KUFANYA MABADILIKO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO NA KOZI ZA VYUO KWA MWAKA 2024

 


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE,2023 KUFANYA MABADILIKO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO NA KOZI ZA VYUO KWA MWAKA 2024



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI

ZA MITAA

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA
KIDATO CHA NNE MWAKA 2023 KUFANYA
MABADILIKO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA
TANO NA KOZI ZA VYUO KWA NJIA YA
MTANDAO KWENYE MFUMO WA KIELEKTRONIKI
WA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA
TANO NA VYUO MWAKA 2024.


Ndugu Wanahabari,
Leo nimewaita hapa kwa ajili ya kutoa taarifa muhimu kwa wahitimu
wa Kidato cha Nne mwaka 2023 kuhusu fursa ya kubadilisha
machaguo ya Tahasusi za Kidato cha Tano na Kozi za Vyuo vya
Ualimu, Vyuo vya Kati na Elimu ya Ufundi kwenye mfumo wa
kielektroniki wa uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na Kidato
cha Tano na Vyuo. Ikiwa ni maandalizi ya awali ya uchaguzi wa
wanafunzi watakaojiunga Kidato cha Tano na Vyuo vya Serikali
Mwaka 2024.

Itakumbukwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fursa kwa wahitimu wa
Kidato cha Nne kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi
(combination) na Kozi mbalimbali walizozichagua kupitia Fomu ya
Uchaguzi (Selform.) Fursa hii huwawezesha wanafunzi
kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye
matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne yaliyotangazwa na Baraza
la Mitihani Tanzania (NECTA).

Ndugu wanahabari,
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imekamilisha zoezi la
awali la kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye Fomu za
Uchaguzi za wanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa
shuleni. Aidha, napenda mtambue kuwa Mabadiliko ya Sera ya



Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala
ya Elimu kwa Kidato cha Tano yameanza kutekelezwa, ambapo
utekelezaji huo umehusisha uanzishaji wa Tahasusi mpya 49,
kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia tahasusi 65.
Tahasusi hizo mpya zitakazoanza kutekelezwa Julai, 2024 zipo
katika makundi saba (7) ambayo ni: Tahasusi za Sayansi ya Jamii;
Tahasusi za Lugha; Tahasusi za Masomo ya Biashara; Tahasusi za
Sayansi; Tahasusi za Michezo; Tahasusi za Sanaa; na Tahasusi za
Elimu ya Dini. Orodha ya masomo na Tahasusi zitakazoanza
kutekelezwa Julai, 2024 (Rejeeni kiambatisho Na.1)
Ndugu wanahabari,
Kukamilika kwa zoezi hili kunatoa fursa kwa wanafunzi kuweza
kufanya mabadiliko ya machaguo/ tahasusi/ kozi kwa njia ya
mtandao (online). Baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao,
kanzidata hiyo ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia
nafasi za Kidato cha Tano na Kozi mbalimbali katika Vyuo vya Kati
na vya Elimu ya Ufundi kwa kuzingatia sifa za ufaulu na machaguo
yao.

Ndugu Wanahabari,
Ofisi ya Rais – TAMISEMI inatoa fursa kwa wahitimu wa Elimu ya
Sekondari Kidato cha Nne mwaka 2023 kubadili machaguo yao ili
kutoa nafasi zaidi kwa Mwanafunzi kusoma tahasusi au kozi



itakayomwandaa kuwa na utaalam stahiki katika maisha yake ya
baadaye. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wakati wa ujazaji wa
fomu za machaguo ya awali, tahasusi mpya 49 hazikuwepo kwenye
orodha ya machaguo na pia matokeo ya mtihani wa kuhitimu Kidato
cha Nne hayakuwa yametoka kumuwezesha mwanafunzi kuweza
kuwa na machaguo mazuri zaidi kulingana na ufaulu wake. Hivyo,
zoezi hili litatoa fursa zaidi ya wanafunzi kuongeza machaguo na
kufanya machaguo mapya ya Tahasusi na Kozi. Napenda kuwasihi
wazazi/walezi kushiriki katika zoezi hili kwa kushauriana na watoto
wao katika kufanya machaguo sahihi kulingana na ufaulu wao.

Ndugu Wanahabari,
Kwa umuhimu huo, wahitimu wote wanahimizwa kufanya
marekebisho ya machaguo ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu
wao, kwa kuingia kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi
(Student Selection MIS) unaopatikana kupitia kiunganishi cha
selform.tamisemi.go.tz. Aidha, maelekezo kwa wahitimu na jinsi
ya kufanya mabadiliko yanapatikana kwenye mfumo wa uchaguzi
wa wanafunzi. Ili kuingia kwenye mfumo itabidi mhitimu atumie
Namba ya Mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2023,
Jina lake la Mwisho, Mwaka wa Kuzaliwa na Alama ya Ufaulu
aliyopata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote
atakaloulizwa.



Ndugu wanahabari,
Ni matumaini yangu kuwa wahitimu wote watatumia kwa ukamilifu
fursa waliyopewa ya kubadilisha Tahasusi na Kozi kulingana na
ufaulu waliopata na kutumia fursa ya kuchagua tahasusi mpya
zitakazoanza kufundishwa Julai, 2024. Pia wataweza kusoma
tahasusi/kozi ambazo wamefaulu vizuri ama wana malengo nazo
zaidi.

Zoezi la kubadilisha tahasusi na vyuo litaanza rasmi tarehe
20 Machi, 2024 hadi tarehe 30 Machi, 2024. Wanafunzi, wazazi na
walezi wanakumbushwa kushauriana kikamilifu ikiwa ni pamoja na
kupata ushauri wa kitaalam na kitaaluma kabla ya kufanya
mabadiliko ya tahasusi au Kozi.

Ninawasisitiza wanafunzi, wazazi/ walezi kutumia muda huo vyema
ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza mara baada ya
matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha
Tano na Vyuo kutangazwa. Ni muhimu kuzingatia muda uliotolewa
wa kufanya marekebisho ili ratiba ya kuwachagua na kuwapangia
shule na vyuo iweze kuendelea kwa muda uliopangwa. Baada ya
matokeo ya kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa,
Ofisi haitashughulikia changamoto hizo kwa kuwa fursa ya
kufanya mabadiliko hayo imeshatolewa.



Huduma hii ya kubadilisha tahasusi ni bure na endapo
wanafunzi watapata changamoto, wawasiliane na Dawati la
Huduma la Mteja kupitia barua pepe: huduma@tamisemi.go.tz
au kuwasiliana moja kwa moja na Kituo cha Huduma kwa
Wateja kwa simu +255 262 160 210 na +255 735 160 210. Aidha,
pamoja na maelekezo hayo, kwa mwanafunzi, mzazi/mlezi
atakayekuwa na suala linalohitaji maelezo au ufafanuzi zaidi
aende katika Ofisi za Elimu za Mikoa na Halmashauri.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Mhe. Mohammed O. Mchengerwa, (MB)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS
(TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA)



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

ORODHA YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO ZITAKAZOTUMIKA

KUANZIA MWEZI JULY,2024

Na. MASOMO

A: TAHASUSI ZA SAYANSI YA JAMII

1 History, Geography and Kiswahili (HGK)
2 History, Geography and English Language (HGL)
3 History, Geography and French (HGF)
4 History, Kiswahili and English Language (HKL)
5 History, Geography and Arabic (HGAr)
6 History, Geography and Chinese (HGCh)
7 History, Geography and Economics (HGE)
8 History, Geography and Fasihi ya Kiswahili (HGFa)
9 History, Geography and Literature in English (HGLi)
B: TAHASUSI ZA LUGHA

10 Kiswahili, English Language and French (KLF)
11 Kiswahili, English Language and Arabic (KLAr)
12 Kiswahili, English Language and Chinese (KLCh)
13 Kiswahili, Arabic and Chinese (KArCh)
14 Kiswahili, Arabic and French (KArF)


15 English Language, French and Arabic (LFAr)
16 English Language, French and Chinese (LFCh)
17 French, Arabic and Chinese (FArCh)
18 History, English Language and French (HLF)
19 History, English Language and Arabic (HLAr)
20 History, English Language and Chinese (HLCh)

C: TAHASUSI ZA MASOMO YA BIASHARA

21 Economics, Business Studies and Accountancy (EBuAc)
22 Economics, Geography and Mathematics (EGM)
23 Economics, Commerce and Accountancy (ECAc)
24 Economics, Computer Science and Mathematics (ECsM)
25 Business Studies, Accountancy and Computer Science (BuAcCs)
26 Business Studies, Accountancy and Mathematics (BuAcM)
27 Economics, Business Studies and Islamic Knowledge (EBuI)
D: TAHASUSI ZA SAYANSI

28 Physics, Chemistry and Mathematics (PCM)
29 Physics, Chemistry and Biology (PCB)
30 Physics, Geography and Mathematics (PGM)
31 Chemistry, Biology and Geography (CBG)
32 Physics, Mathematics and Computer Science (PMCs)
33 Chemistry, Biology and Agriculture (CBA)
34 Chemistry, Biology and Food and Human Nutrition (CBN)



E: TAHASUSI ZA MICHEZO
35 Biology, Food and Human Nutrition and Sports (BNS)
36 English Language, Music and Sports (LMS)
37 Kiswahili, Music and Sports (KMS)
38 Fasihi ya Kiswahili, Music and Sports (FaMS)
39 Literature in English, Music and Sports (LiMS)
40 French, Music and Sports (FMS)
41 Arabic, Music and Sports (ArMS)

F: TAHASUSI ZA SANAA

42 Kiswahili, English Language and Theatre Arts G(KLT)
43 Kiswahili, French and Theatre Arts (KFT)
44 Fasihi ya Kiswahili, English Language and Theatre Arts (FaLT)
45 Kiswahili, Literature in English and Theatre Arts (KLiT)
46 Kiswahili, English Language and Music (KLM)
47 Kiswahili, French and Music (KFM)
48 Fasihi ya Kiswahili, English Language and Music (FaLM)
49 Kiswahili, Literature in English and Music (KLiM)
50 Kiswahili, English Language and Fine Art (KLFi)


51 Kiswahili, French and Fine Art (KFFi)
52 Fasihi ya Kiswahili, English Language and Fine Art (FaLFi)
53 Kiswahili, Literature in English and Fine Art (KLiFi)
54 Kiswahili, Textile and Garment Construction and Fine Art (KTeFi)
55 English Language, Textile and Garment Construction and Fine Art (LTeFi)
56 Arabic, Textile and Garment Construction and Fine Art (ArTeFi)
57 Chinese, Textile and Garment Construction and Fine Art (ChiTeFi)

G: TAHASUSI ZA ELIMU YA DINI

58 Islamic Knowledge, History and Geography (IHG)
59 Divinity, History and Geography (DHG)
60 Islamic Knowledge, History and Arabic (IHAr)
61 Divinity, History and English Language (DHL)
62 Islamic Knowledge, History and English Language (IHL)
63 Divinity, History and Kiswahili (DHK)
64 Islamic Knowledge, History and Kiswahili (IHK)
65 Divinity, Kiswahili and English Language (DKL)

No comments:

Post a Comment